Habari

Siri ya Mutungi na Lipumba yavuja

Chanzo: jamhuri ya Zanzibar – Jamii Forums
Jumamosi, Februari 16, 2019

(Jaji Benhajii ategwa kuvuruga Mashauri ya CUF No. 13/2017 na No. 23/2016)​

Tarehe 5/8/2015 aliyekuwa mwenyekiti wa chama cha CUF Prof. Ibrahimu Haruna Lipumba alitangaza kupitia vyombo vya habari kung’atuka rasmi nafasi ya uenyekiti wa CUF-Chama cha Wananchi na siku hiyo hiyo alikabidhi barua ya kung’atuka kwake kwa Katibu Mkuu wa Chama Maalim Seif Sharif Hamad.

Pamoja na kwamba kujiuzulu kwake hakukutarajiwa kutokana na kwamba tayari Chama kilikuwa katika mchakato wa maandalizi ya uchaguzi mkuu wa nchi wa Oktoba, 2015, lakini kwa kuzingatia Katiba ya Chama ya mwaka 1992 (Toleo la 2014) ibara ya 117(1), uamuzi huo ulikuwa halali na uliheshimika.

Kwa kuzingatia mazingira ya kipindi hicho kuelekea uchaguzi mkuu wa nchi, na hali ya ofisi za Mwenyekiti na Makamo Mwenyekiti kuwa wazi, Baraza Kuu la Uongozi la Taifa liliunda Kamati ya Uongozi chini ya ibara ya 101 ikiongozwa na Mhe. Twaha Issa Taslima kusimamia Chama katika kipindi hicho cha mpito kabla ya kuitishwa kwa Mkutano Mkuu wa Taifa kuridhia kung’atuka kwa Lipumba ikizingatiwa matakwa ya ibara ya 117(2) ya Katiba ya CUF.

Mkutano Mkuu wa Taifa uliitishwa na Baraza Kuu la Uongozi la Taifa tarehe 21/8/2016 na wajumbe 659 walipiga kura; ambapo jumla ya wajumbe 476 (kiwango cha 72.23%) waliridhia kung’atuta kwa Prof. Ibrahim Haruna Lipumba.

Hata hivyo katika hali isiyotegemewa msajili wa vyama vya siasa ambaye ni Jaji wa Mahakama Kuu Francis Katabazi Mutungi, aliandika barua tarehe 23/9/2019 ya kumtambua Lipumba kuwa ni mwenyekiti halali wa CUF-Chama cha Wananchi na kumwombea ulinzi wa Polisi kwa Inspekta Generali wa Polisi (IGP) ambaye alitoa gari mbili (defender) za askari wenye silaha waliomwezesha Lipumba na genge la wahuni kuvamia Ofisi Kuu ya CUF iliyoko Bugururni Dar es salaam na kuingia ndani kwa kuvunja milango siku ya Jumamosi ya tarehe 24/9/2016.

Uamuzi huo wa Msajili wa vyama vya siasa ndio uliozaa kile kinachoitwa “mgogoro wa uongozi ndani ya CUF”.

Mpango huo ulioratibiwa na dola kwa kumtumia msajili wa vyama vya siasa ulitegemea kuwa wanachama na viongozi wa CUF wakiongozwa na Katibu Mkuu Maalim Seif Sharif Hamad wangelikwenda kumtoa Lipumba Buguruni kwa nguvu ili wapate sababu ya kufanya mauaji kwa kutumia polisi (defender mbili za askari wenye silaha) na hivyo kumkamata Maalim Seif na viongozi wenzake kuwafungulia mashtaka ya mauaji ambayo yangewalazimu kukaa ndani kwa miaka na hivyo kumwezesha Lipumba kuwapatia CCM chama kibaraka kitakachokubali kuihalalisha serikali haramu ya Dk. Ali Mohamed Shein.

Busara za viongozi wa CUF ziliona mbali, na kuamua Bodi ya Wadhamini ya CUF-Chama cha Wananchi; ambayo ndio mdomo wa kisheria wa chama, kufungua shauri Na. 23/2016 tarehe 19/10/2016 Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Kuu ya Dar es salaam ikihoji mamlaka ya msajili wa vyama vya siasa kumtambua kama kiongozi mtu ambaye aliamua kujiuzulu mwenyewe, kuwa nje ya ofisi kwa takriban miezi kumi na kujiuzulu kwake kuthibitishwa na Mkutano Mkuu wa Taifa.

Aidha kutokana na kiburi alichokuwa anapewa na msajili wa vyama vya siasa na dola, Lipumba aliendelea kufanya hujuma nyingine nyingi dhidi ya Chama na Wanachama ikiwemo kusajili Bodi feki ya Wadhamini kwa nyaraka za kughushi, kuwafukuza Wabunge, Madiwani, viongozi wa serikali za mitaa na wa Chama ngazi mbali mbali na hivyo Bodi ya Wadhamini na wanachama walioathirika waliendelea kufungua mashauri mengine mahakamani. Kwa ujumla na kwa nyakati tofauti, takriban mashauri 37 yalifunguliwa.

Mkono wa dola kuingilia uhuru wa muhimili wa mahakama ulianza kuonekana tangu mwanzo kupitia shauri Na. 23/2016, ambapo Jaji Sekieti Suleiman Said Kihio aliyepangwa kusikiliza shauri hilo siku ya kwanza kabisa, alisikika hadharani akiwaelekeza wadaiwa (Respondents) kuweka hoja za pingamizi la awali (points of preliminary objection) kuwa Bodi ya CUF-Chama cha Wananchi sio hai.

Siku ya pili ya kuitishwa shauri hilo wadaiwa (mwanasheria mkuu wa serikali) aliweka pingamizi hilo hilo linalohoji uhai wa Bodi ya Wadhamini). Ilishangaza sana kumsikia kutamka maneno hayo jaji anayetegemewa kuwa mtu wa kati (impartial/neutral).

Hali hiyo ilitahadharisha kuwa tayari kuna mawasiliano yanaendelea kati ya jaji na upande kinzani (Respondents) na hivyo Bodi ya Wadhamini iliamua kumwandikia barua ikimtaka ajitoe kusikiliza shauri hilo.

Hata hivyo Jaji Sekieti Suleiman Said Kihio aligoma kujitoa jambo lililosababisha Bodi kuomba marejeo (Revision) Mahakama ya Rufaa. Mahakama ya Rufaa ilitoa kibali kwa Bodi ya Wadhamini kuomba marejeo, lakini kabla ya hatua hiyo, jaji Kihio alistaafu na ndipo shauri likapangwa kwa jaji Ignus Kitusi kuendelea nalo Mahakama Kuu.

Katika hali ya kushangaza Jaji Ignus Kitusi aliendelea kulihairisha bila kulisikilizwa kwa takriban miezi sita mpaka alipohamishwa mwezi Julai, 2018.

Nguvu kubwa ya dola ilitumika na taarifa zilionyesha kuwa majaji walianza kutishwa na usalama wa Taifa (TIS), wakishinikizwa kutupilia mabali mashauri yote dhidi ya msajili wa vyama vya siasa na Lipumba kupitia hoja za awali (points of preliminary objection).

Kwa ushahidi wa kimazingira, baadhi ya majaji walionekana kutishika na waliendelea kuhairisha kusikilizwa kwa mashauri kwa kipindi kirefu isipokuwa Jaji Wilfred Dyansobera aliyesimamia kiapo chake na kuongozwa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ibara ya 107.

Kwa msimamo huo wa Jaji Dyansobera, Lipumba akiwatumia watu wake Peter Michael Malebo na Thomas D. C. Malima alimwandikia barua (Kumb. Na. CUF/AK/RPP/27/2017 ya tarehe 27/10/2017) Jaji Mkuu kumtaka amuondoe Jaji Wilfred Dyansobera kusikiliza mashauri dhidi yao.

Hatua hiyo ilikolezwa na wakili mkuu wa serikali Gabriel Malata aliyemuamuru hadharani Jaji Wilfred Dyansobera kuzingatia maelekezo yake wakati wa kusikiliza mashauri ya CUF; aliyodai yalitolewa na Rais John Pombe Joseph Magufuli.

Kilichofuata baada ya kauli hiyo ya wakili mkuu wa serikali ni uhamisho wa ghafla wa majaji wote sita waliokuwa wanasikiliza mashauri ya CUF na kuagizwa kukabidhi mara moja mafaili ya kesi hizo kwa Jaji Kiongozi ili awapangie majaji wengine wapya watakaoletwa.

Taarifa zinaonyesha lengo lilikuwa kumwondosha Jaji Dyansobera lakini kufanya siri hiyo isivuje ikalazimika kufanya uhamisho wa majaji wote ili ionekane ni uhamisho wa kawaida.

Kwa takriban miezi miwili Julai – Septemba 2018 kesi zote za CUF zilisimama na katika kipindi hicho mafaili ya kesi za CUF yalionekana katika jengo moja mitaa ya Lumumba yakiwa mikononi mwa usalama wa Taifa (TIS) waliopewa kazi maalum ya kuyachunguza ili kuona kama kuna namna ya kupindisha maamuzi ya mahakama (judgment) iwapo mashauri yatasikilizwa mpaka mwisho.

Hata hivyo ilionekana jambo hilo ni gumu na ndiyo maana ikapendekezwa apatikane jaji anayeweza kushawishika (compromised) apewe kazi hiyo.

Majaji waliokuwa wanasikiliza mashauri ya CUF na waliokumbwa na kadhia ya uhamisho ni hawa wafuatao;

Ignus Kitusi
Jugano Samson Mwandambo
Rehema Kerefu Sameji
Nkasimonga, J
Muruke, J
Wilfred Dyansobera

Mmoja wa majaji wapya waliopangwa kusikiliza mashauri ya msingi ya CUF ni Jaji Dk Benhajj Shaaban Masoud (aliyetolewa Mahakama Kuu kanda ya Tanga). Mashauri aliyopangiwa ni Na. 23/2016 (linalohoji mamlaka ya msajili wa vyama vya siasa kumtambua Lipumba na kuingilia vikao vya kikatiba vya Chama), Na. 13/2017 (juu ya usajili wa Bodi feki ya wadhamini).

Na shauri Na. 143/2017 (linalopinga kufukuzwa wabunge wanane Viti Maalum). Pia alipangiwa shauri Na.40/2018 (linalopinga uitishwaji wa mkutano mkuu feki kwa lengo la kumfukuza Katibu Mkuu Maalim Seif Sharif Hamad na viongozi wengine waandamizi wa chama).

Jaji Masoud amesikilza mashauri yote hayo na kupanga kutoa hukumu tangu tarehe 12 Oktoba, 2018 lakini amekuwa akihairisha kusomwa hukumu kwa visingizio mbali mbali mpaka sasa.

Katika hali ya kushangaza imebainika kuwa sababu ya hairisha hairisha ni mazungumzo yaliyokuwa yanafanyika kati ya Jaji Benhajj, Msajili wa vyama vya siasa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kumshawishi jaji ampatie ushindi kwa hali yoyote ile Lipumba katika mashauri hayo matatu ya msingi.

Mazungumzo hayo yalitokana na kile kilichoelezwa kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano (Rais Magufuli) kuchoshwa na Lipumba ambaye ameonekana habebeki licha ya kusaidiwa kwa kila hali, ikiwemo kuruhusu apatiwe ruzuku ya takriban Tshs.1,076,982,032.12 ambazo hazionekani kutumika ilivyokusudiwa.

Kwa mujibu wa taarifa ya mfuasi wa Prof Ibrahim Lipumba anayeitwa Abdalla Seif (aliyewahi kutia nia kugombea Ubunge Jimbo la Wawi Pemba), Lipumba amewahakikishia wafuasi wake kuwa Msajili amemjulisha kuwa mazungumzo na Jaji Benhajj yamekamilika na gharama aliyotaka ya Tshs. 300,000,000/= imepatikana baada ya Mama Samia Suluhu Hassan (Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano) kutoa Tshs. 150,000,000/= na Balozi Ali Seif Idd (Makamu wa Pili wa SMZ) kutoa Tshs. 200,000,000/=.

Lipumba amesema kuwa tayari Jaji Benhajj Shaaban Masoud amepokea malipo hayo na ataanza kutekeleza makubaliano kwa kutoa hukumu ya shauri dogo la Wabunge Viti Maalum (Shauri Na. 51/2018) ambalo amehaidi kulitupilia mabali kwa gharama licha ya kwamba halina tatizo lolote.

Abdalla Seif ameeleza kuwa Lipumba alitoa kauli hiyo nyumbani kwa Mussa Haji Kombo (Pemba) alikofanya kikao na wafuasi wake mara baada ya kutoka kwenye sherehe za mapinduzi tarehe 12/1/2018 kwa mwaliko wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Aidha Tshs. 14,000,000/= ya bakaa ya Tshs. 50,000,000/= imemwezesha Lipumba kulipa mshahara kwa wafuasi wake ambao miezi kadhaa hawana mshahara kufuatia kusitishwa kwa ruzuku kwa amri ya mahakama.

Jaji Benhajj awali alipanga kusoma hukumu ya shauri hilo tarehe 21/1/2019 lakini siku hiyo badala ya kusoma hukumu alizua jambo la kisheria ambalo halikuwekwa kama pingamizi na upande kinzani (Respondents) na kutaka wasomi mawakili wa pande zote mbili walitolee ufafanuzi ndipo akamilishe hukumu yake na kuisoma siku hiyo hiyo.

Mawakili wa pande zote mbili waliomba muda kujiandaa maana suala hilo halikuwa sehemu ya mabo yanayobishaniwa. Jaji Benhajj aliwapa muda hadi tarehe 24/1/2019.

Licha ya mawakili wa pande zote mbili kukubaliana kuwa shauri Na. 51/2018 lilikidhi vigezo vyote vya kisheria na kutoa ushahidi wa hukumu za majaji kadhaa; wakiwemo Majaji Masati na Magoiga (Septemba, 2018), lakini katika hali isiyotarajiwa Jaji Benhajj Masoud alisimamia hoja yake na kupingana na hukumu za majaji wengine walizotoa kuhusiana na suala hilo na kuwakosoa kwa dhana (in his opinion) bila kuwa na ushahidi wa kisheria.

Hukumu hiyo kwa kiasi fulani imethibitisha kauli ya Lipumba kuwa tayari makubaliano yamefikiwa na hivyo kuna kila dalili ya Jaji Benhajj kuendelea kuzingatia makubaliano na sio sheria katika kutoa uamuzi kwa mashauri ya msingi yaliyobakia; amabyo amepanga kusoma hukumu zake tarehe 18/2/2019 (Shauri Na. 13/2019) na 22/2/2019 (Shauri Na. 23/2016).

Baada ya hukumu hiyo ya shauri Na. 51/2018, wakili wa Lipumba msomi Mashaka Ngole aliendelea kuthibitisha kauli iliyotolewa na Abdalla Seif; kuhusu makubaliano kati ya Jaji Benhajj na Msajili, jambo linalothibitisha kuwa taarifa ya Lipumba kwa wafuasi wake aliyoitoa Pemba tarehe 12/1/2019 ina ukweli.

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imekuwa mfadhili mkubwa wa Lipumba kutokana na makubaliano kuwa akipewa CUF ataitambua mara moja serikali haramu ya Dk Ali Mohamed Shein na hivyo kuhalalisha uharamia uliofanywa na serikali ya Rais Jakaya Mrisho Kiwete kutumia vyombo vya ulinzi na usalama vya Jamhuri ya Muungano kupora ushindi wa mshindi halali wa uchaguzi wa Oktoba 25, 2015 Maalim Seif Sharif Hamad (Katibu Mkuu wa CUF-Chama cha Wananchi).

Katika uchaguzi huo Maalim Seif Sharif Hamad alipata kura 207,847 dhidi ya mgombea wa CCM, Dk Ali Mohamed Shein, aliyeambulia kura 182,011. CUF pia ilifanikiwa kuongeza majimbo yake kisiwani Unguja kutoka manne (4) hadi tisa (9) mbali ya kuendelea kubakisha majimbo yake yote 18 kisiwani Pemba.

Mafanikio haya na ushindi huu mkubwa umekuwa mwiba kwa watawala na ndiyo hujuma zote hizi zinatelekezwa ili kuisambaratisha CUF. Kinachoitisha CCM; hususan, viongozi wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, ni kuwa tangu mwaka 1995 licha ya nguvu kubwa ya dola inayotumika wakati wa uandikishwaji wa wapiga kura na uchaguzi wenyewe, CUF imaendelea kuongeza ushindi wake.

Hivyo mara hii wameamua kuwekeza kwa Lipumba kuisambaratisha nguvu ya CUF na kinyume na fikra zao kuwa njia hii ilikuwa salama, wamegundua kuwa sheria ikisimama hakuna kesi ambayo Lipumba anaweza kushinda. Hivyo mazungumzo na jaji Benhajj ndiyo yameonekana kuwa na tija licha ya kutaka gharama kubwa.

Hata hivyo muhimu Majaji wa Mahakama za Tanzania; hususan Jaji Benhajj Shaaban Masoud, kujitathmini kuona kama wanafaa kuendelea na kazi hiyo ya ujaji katika mazingira hayo.

Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Tanzania, ibara za 107A na 107B Mahakama ndicho chombo cha utoaji haki na katika kutekeleza jukumu hilo haipaswi kuingiliwa na serikali, Bunge wala Baraza la Wawakilishi, haitajali hali ya mtu kijamii na kiuchumi, haitachelewesha haki bila sababu za msingi na itaendeleza usuluhishi baina ya pande zenye mgogoro.

Aidha katika kutekeleza jukumu hilo, mahakama itazingatia masharti ya katiba na yale ya sheria za nchi. Jaji ambaye hawezi kutafsiri masharti hayo ya katiba ya nchi na kuyazingatia, ni bora akafanye kazi nyingine maana anaelekea kuipeleka nchi katika maafa makubwa. Mahakama Kuu ya India katika kesi ya Gupta dhidi ya Rais wa nchi hiyo mwaka 1982 ilitamka ifuatavyo;

“the constitution is an organic instrument intended to endure and its provisions must be interpreted having regard to the constitutional objectives and goals and not in the light of how a particular Government may be acting at a given point of time.

Judicial response to the problem of constitutional interpretation must no suffer from the fault of emotionalism or sentimentalism which is likely to cloud the vision when judges are confronted with issues of momentous importance”

Kwa tafsiri isiyo rasmi;

“Katiba ni kiumbe kinachotegenewa kuishi, na hivyo ibara zake zinapaswa kutafsriwa kwa kuzingatia malengo na dhamira yake na si kutokana na serikali inavyoweza kuwa inataka wakati fulani.

Jukumu la mahakama wakati wa kuitafsiri katiba lisibughudhiwe na mihemuko na ubinafsi mambo ambayo hupofusha majaji wanapokabiliwa na mambo yenye maslahi muhimu.”

Ni hatari maofisa wa mahakama (majaji) kujiingiza katika matendo ya rushwa yanayokinzana na maadili ya watumishi wa muhimili wa mahakama. Kanuni ya kwanza (Rule-1) ya maadili ya maofisa wa mahakama (1984) inawataka kuzingatia sheria za nchi na watende kwa jinsi ya kukuza imani, heshima na uhuru wa mahakama.

Afisa wa mahakama atakuwa anakiuka maadili ya kazi yake akiruhusu familia, jamii au mahusiano mengine kuingilia utendaji (conduct) na maamuzi (judgment) yake kwa maslahi binafsi. Maafisa wa mahakama wanahimizwa kutoruhusu kueleweka au kufanywa na wengine kueleweka kuwa wanashawishika.

Kimsingi hata utawala wa sheria katika nchi yoyote unategemea utendaji wa mahakama. Mahakama ambayo maafisa wake hawazingatii maadili ya kazi zao inaweza kuwa sababu ya nchi kuingia katika maafa makubwa. Rais wa 32 wa Marekani (1882 – 1945) Franklin Delano Roosevelt aliwahi kusema;

“The greatness of a nation lies in its fidelity to its constitution and strict adherence to the rule of law and above all the fear of God”

Jaji Benhajj ajitafakari kama utendaji wake unaakisi kuzingatia katiba ya nchi, sheria za nchi na kama anayo hofu ya Mungu ili kuhakikisha kuwa Taifa letu linakuwa kuu miongozi mwa mataifa mengine duniani. Labda vizuri piqa kumkumbusha Jaji Benhajj Shaaban Masoud kuwa asikubali kupotosha haki kwa kutishwa na hao anaowaita serikali. Selikali ni watu waliowaweka hao viongozi wanaomtisha. Franklin Roosevelt aliwahi kusema;

“Let us never forget that government is oueselves and not an alien power over us. The ultimate rulers of our democracy are not President and senators and congressmen and government officials, but the voters of this country.”

Katika hatua nyingine, msajili wa vyama vya siasa tayari ameingizia takriban Tshs. 1,000,000,000/= katika akaunti Na. 2072300456 ya NMB Temeke ikiwa ni maandalizi ya kumwezesha Lipumba kuitisha Mkutano Mkuu mara baada ya Jaji Benhajj kuwatangazia ushindi.

Mkutano Mkuu huo ulipangwa kuitishwa mwezi Mei, 2018, lakini kwa kiasi umezuiwa na mahakama kufuatia kufunguliwa kwa shauri Na. 40/2018 lilolopo mbele ya Jaji Benhajj.

Kwa sasa Lipumba ameziandikia barua wilaya zote za Tanzania Bara ambazo ziligomea uchaguzi wake batili kufanya hivyo haraka ili kuweza kushiriki Mkutano Mkuu huo unaotarajiwa wakati wowote mwezi Machi, 2019. Maandalizi hayo yote yanathibitisha kwa kiasi kikubwa usahihi wa taarifa ya Abdalla Seif iliyothibitishwa na wakili Mashaka Ngole.

HII NDIYO AWAMU YA HAPA KAZI TUU INAYOPAMBANA NA RUSHWA NA UFISADI

Tagsslider
Share: