Habari

Spika aunda kamati 7 za kisekta Zanzibar

April 17, 2016

Na, Himid Choko, BLW.

SPIKA wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Zubeir Ali Maulid ameunda Kamati saba (7) za Kudumu za kisekta za Baraza la wawakilishi , ili kuhakikisha kwamba Baraza hilo linatekeleza kwa ufanisi mkubwa zaidi Kazi ya kuisimiamia serikali.

Katibu wa Baraza la Wawakilishi Dkt Yahaya Khamis Hamad amesema Spika Maulid ameunda Kamati hizo kwa mujibu wa Kanuni ya 107 (1) (a) ya Baraza la Wawakilishi Toleo la 2012.

Amesema kwa mujibu wa Kanuni hiyo mjumbe yeyote wa Baraza asiyekuwa Makamu wa Pili wa Rais, Waziri, Naibu Waziri au Mwanasheria Mkuu anaweza kuteuliwa kuwa Mjumbe wa Kamati ya Kudumu yeyote inayohusika na Kanuni za Baraza.

Dkt Yahya amezitaja Kamati hizo kua ni ile ya Kusimamia Ofisi za Viongozi Wakuu wa Kitaifa, ambayo itahusika na Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pamoja na Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais. Wajumbe wa Kamati hii wamemchagua Omar Seif Abeid ( Konde) kuwa Mwenyekiti na Panya Ali Abdullah (Viti Maalum) kuwa Makamo Mwenyekiti.

Wajumbe wengine wa Kamati hii ni Amina Idd Mabrouk (Viti Maalum), Mtumwa Suleiman Makame (Viti Maalum) , Simai Mohammed Said (Tunguu) , Mohammed Said Dimwa (Mpendae), Hussein Ibrahim Makungu (Mtoni) na Mussa Ali Mussa (Ole) . Awali katika Baraza lililopita Kamati hii ilikua ikiongozwa na Hamza Hassan Juma akiwakilisha Jimbo la Kwamtipura.

Kamati nyengine ni ya Sheria na Utawala, ambayo inahusika na Ofisi ya Rais, Katiba, Utumishi wa Umma na Utawala Bora na Wizara ya Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ ambapo wajumbe wa Kamati hiyo wamemchagua aliyewahi kuwa Waziri na Mjumbe wa Baraza la Mapinduzi katika awamu zilizopita Machano Othman Said (Mfenesini) kuwa Mwenyekiti wake na Mwantatu Mbarak Khamis (Viti Maalum), kuwa Makamo Mwenyekiti.

Wajumbe wengine wa Kamati ya Katiba Sheria na Utawala ni pamoja na Saada Ramadhan Mwenda ( Viti Maalum), Wanu Hafidh Ameir (viti Maalum), Mihayo Juma N,hunga (Mwera), Shamata Shaame Khamis ( Micheweni), Nadir Abdullatif Yussuf (Chaani) na Ali Khamis Bakari(Tumbe).

Dkt. Yahya amesema aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Kusimamia Ofisi za Viongozi Wakuu wa Kitaifa katika Awamu iliyopita , Hamza Hassan Juma (Shauri Moyo) ameendelea kutumikia wadhifa huo katika Kamati ya Mawasiliano na Ujenzi ambayo itahusika na Wizara ya Ardhi , Maji, Nishati na Mazingira pamoja na Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji .

Amesema Kamati hiyo ya Mawasiliano na ujenzi pia imemchagua Suleiman Sarhan Said (Chakechake) kuwa Makamo mwenyekiti wake . Wajumbe wengine wanaounda Kamati hiyo ni pamoja na Mohammedraza Hassanali Mohammedali (Uzini), Abdullah Ali Kombo (Mwanakwerekwe), Mwanaidi Kassim Mussa (viti maalum), Khadija Omar Kibano (Mtambwe), Bahati Khamis Kombo (Chambani), Nassor Salim Ali (Kikwajuni), na Said Omar Said (Wingwi),

Kamati nyengine ni Kamati ya Maendeleo ya wanawake na Ustawi wa Jamii ambayo imemchagua aliyekuwa Waziri katika Awamu zilizopita Dr. Mwinyihaji Makame (Dimani) kuwa Mwenyekiti na Tatu Mohammed Ussi kuwa Makamo Mwenyekiti wa kamati hiyo.

Wajumbe wengine wa Kamati hii ambayo itahusika na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali pamoja na Wizara ya Afya ni Viwe Khamis Abdullah( Viti Maalum), Hidaya Ali Makame ( Viti Maalum), Mwanaasha Khamis Juma ( Chukwani) , Masoud Abrahman Masoud ( Bububu) , Ame Haji Ali ( Nungwi) na Makame Said Juma (Kojani).

Kwa upande wa Kamati ya Kuchunguza na Kudhibiti Hesabu za Serikali na Mashirika (PAC) inaongozwa na Miraji Khamis Mussa (Chunbuni) na Makamo Mwenyikiti wake ni Shaib Said Shaib (Chonga) , Wajumbe wengine ni Mtumwa Peya Yussf (Bumbwini), Zainab Abdullah Salum (Viti Maalum), Dr. Makame Ali Ussi( Mto pepo), Abdullah Maulid Diwani Jang”ombe), Zulfa Mmaka Omar (Viti Maalum).

Kamati ya Fedha, Biashara na Kilimo inayohusika na Wizara ya Fedha na Mipango, Wizara ya biashara, Viwanda na Masoko pamoja na Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi inaongozwa na Yussuf Hassan Idd ( Fuoni ) na Makamo mwenyekiti wake ni Hamida Abdullah Issa ( Viti Maalum). Wajumbe wengine wa Kamati hii ni Ussi Yahya Haji (Mkwajuni), Bihindi Khamis Hamad (Viti Maalum), Shadya Mohammed Suleiman ( Viti Maalum) , Ali Salum Haji (Kwahani), Hamad Abdullah Rashi(Wawi), na Mohammed Mgaza Jecha( Mtambile).

Dkt Yahaya ameitaja Kamati ya mwisho kuwa ni ile ya Mifugo, Utalii, Uwezeshaji na Habari itakayohusika na Wizara ya Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo pamoja na Wizara ya Kazi, Uwezeshaji , Wazee , Vijana , Wanawake na Watoto. Amesema kamati hiyo itaongozwa na Ali Suleiman Ali( Kijitoupele) na Makamo Mwenyekiti wake ni Salha Mohammed Mwinjuma (Viti Maalum).

Wajumbe wengine ni Zainab Abdullah Salum ( Viti Maalum), Asha Abdullah Mussa (Kiwengwa), Jaku Hashim Ayoub( Paje), Suleiman Makame Ali (Ziwani), Mussa Foum Mussa( Kiwani), Hassan Khamis Hafidh ( Welezo) na Maryam Thani Juma (Gando).

Mwisho

Share: