Habari

Swali kwa Mh. Othman Masoud

Tumeona pendekezo lako juu ya muundo mpya wa Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania.

Naomba ninukuu sehsmu insyosema:

“Sehemu moja iwe na wajumbe kutoka Tanzania Bara pekee na ishughulikie mambo yasiyo ya Muungano kwa Tanzania Bara na sehemu ya pili iwe na idadi ndogo ya wabunge kwa idadi sawa kutoka pande mbili za Muungano na ishughulikie mambo ya Muungano pekee,”

Swali langu mheshimiwa ni kwamba, chombo gani kitakacholipia gharama zote za hii seshsmu ya Bunge litakaloshughulikia mambo ya Tanganyika yasiyo ya muungano?

Kwa sababu hakuna serikali ya Tanganyika. Na haziwezi kulipiwa na serikali ya Muungano kwa sababu shughuli zake hazihusiani na Jamuhuri ya muungano.

Na kama zitalipiwa na Jamhuri ya Muungano ni lazima na gharama zote za Baraza la Wawakilishi la Zanzibar zilipiwe na Jamhuri ya Muungano. Vyenginevyo nipe maelezo.

Share: