Habari

Swali langu kwako Mzee Kondo

Kwa mujibu wa kumbukumbu zangu Tume ya uchaguzi ya Zanzibar chini ya Mwenyekiti Mwinchande ilikabidhi ripoti yake ya uchaguzi tarehe 27 Decemder 2012. Ikiashiria kuwa inafikia ukingoni mwa uhai wake. Pia nakumbuka kuwa December 31 2012 ilifika mwisho wa utumishi wake ambapo kwa lugha nyengine tulisema ime EXPIRE.

Pia nakumbuka kuwa kamisheni ya Tume mpya ya uchaguzi ilitangazwa katika mwezi wa January mwaka 2013, ikimtambulisha Jecha Salim Jecha kuwa ndio mweyekiti mpya wa ZEC, halkadhalika, kuwatangaza makamishna wa Tume ya uchaguzi ambao walikuwa wawili kutoka CCM, wawili kutoka CUF, na wawili wakitoka kwa Rais wa Zanzibar.

Ingawa Jecha Salim Jecha alikuwa uteuzi wa Rais, twaweza sema alikuwa chaguo la Rais, akiongezwa na hawa wawili wengine, hivyo Rais alikuwa na makamishna 3 kwenye Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar. Huu ni utuezi wa moja kwa moja (directly appoint). Wakati nyuma yake kuna hao wawili ambao wanatoka Chama cha Rais mwenyewe anashiriki kwenye uteuzi wake.

Hoja yangu iko hapa, jee hii Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar chini ya mweyekiti Jecha Salim Jecha lini ina EXPIRE?
Na kutakuwa na utaratibuni wa uteuzi wa makamishna wapya wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar?
Ikiwa Rais wa Zanzibar aliapishwa rasmi kushiika madaraka ya urais tarehe 24 March 2016, jeee kutakuwa na uchaguzi October 2020, au tutasubiri akamilishe term ya miaka yake 5. Kinyume chake atakuwa ametawa miaka 4 na ushei.

Natumai kupata majibu ya ufasaha kutoka kwako Mzee Kondo, hasa kwa vile uko karibu na i muasisi wa sera, itikadi na ilani za chama chako CCM, chama tawala

Share: