Habari

Taarifa ya Mkutano Mkuu ZAWA-UK


Wazalendo na wapenda maendeleo.

Nachukuwa nafasi kuwajulisha na kuwaalika Wananchi wote wanaoishi Nchini Uiengereza, kuhudhuria Mkutano Mkuu wa ZAWA-UK.

ZAWA-UK ni jumuiya iliyoandikishwa na Charity Commission ya Uingereza kufanya kazi za NGO. Lengo lake ni kulinda na kuendeleza haki za Wazanzibar na watu wengine, pamoja na kutoa msaada unaohitajika kwa wanachama wake. Vilevile ni kuisaida nchi ya Zanzibar kimaendeleo.

Mkutano utakuwa siku ya JUMAMOSI, tarehe 26 May 2012, saa 8 mchana hadi saa 11.30 jioni.
Ukumbi utakuwa Gandhi Room, Froud Centre, Manor Park, E12 5JF.

Mada za mkutano ni:
1) Semina kuhusiana na Health living – elimu kwa jamii juu ya afya na matatizo yanayoikumba jamii yetu
2) Taarifa ya jumuiya kwa mwaka 2011/2012
3) Uchaguzi Mkuu wa viongozi wa jumuiya

Kutakuwa na nafasi za uongozi kwa yoyote yule anayetaka kugombea anakaribishwa.

Wote kwa pamoja, tunaomba ujumbe huu tuufikishe kwa kila tunayemjuwa.

Ahsante
Ahmed
Naibu Kyatibu

Share: