Habari

TAARIFA YA NGOME YA VIJANA ACT –WAZALENDO JUU YA UJIO WA WANACHAMA WAPYA

TAARIFA YA NGOME YA VIJANA ACT –WAZALENDO JUU YA UJIO WA WANACHAMA WAPYA

Kama mnavyojua chama chetu kinaendelea kupokea Wanachama wapya kutoka kila kona ya nchi tangu siku ya tarehe 18/03/2019 ambapoViongozi mbalimbali Waandamizi wa chama cha CUF wa kiongozwa na Ndugu Maalim Seif Shariff Hamad walipo tangaza kuachana na kilichokuwa chama chao (CUF) na kujiungana ACT-WAZALENDO.

Leo hii sisiVijana wa ACT WAZALENDO tunatumiafursa hii kuwakaribisha rasmiWanachama na viongozi hawaWaandamizi katika siasa za nchi yetu.Tumepokea ujio wao kwa mikono yote miwili na kwa furaha iliyopitiliza katika mioyo yetu. Tunawapongeza kwa maamuzi yao yakujiunga kwenye chama hiki imara cha ACT-WAZALENDO.Kwa pamoja tunaendeleza mapambano ya haki na democrasia katika nchi yetu.

Kwa namna ya pekee tunampongeza nakumkaribisha Ndugu Maalim Seif katika safari hii mpya ya mapambano kupitia ACT-WAZALENDO. Uamuzi wake wakujiunga nasi, unamaana kubwa sana kwetu sisi Vijanawa ACT –WAZALENDO.

Hebutufikirie, Tanzaniaina vyama vyenye umri mkubwa zaidi yetu visivyopungua 20. Kwa mwanasiasa shupavu, imara, mpambanaji, mtetea haki, asiyeyumbishwa, jasirina Jemedali mwenye historia ndefu na isiyoweza kufutika katika nchi yetu, Kuamua kujiunga na sisi ni kitu kilichofikiriwa na wengi kuwa hakitowezekana. Bahati nzuri ndugu Maalim Seif Shariff Hamad alitueleza sababu za yeye na wenzake kuamua kuichagua ACT-WAZALENDO kama uwanja mpya
wa mapambano.

Ndugu Wanahabari, Sisi vijana wa ACT-WAZALENDO, tunamhakikishia Ndugu Maalim Seif na Wanachama wote wengine wanaojiungana chama chetu kuwa tupo pamoja nao na hakika hawawezi kujutia uamuzi wao wa kujiunga na ACT-Wazalendo.

Kwa namna ya kipekee tunatoa pongezi kwa chama kwa kumpatia kadi no 1 ndugu Maalim SEIF. Ni uamuzi sahihi na umekipambanua chama chetu kama chama cha kila Mtanzania na kisichona ubaguzi wa aina yeyote. Kwa mapambano aliyoyafanya Mzee wetu Maalim Seif ya kutetea haki na wanyonge kwa kipindi kirefu cha maisha yake alistaili kutunukiwa na taifa. Vijana wa ACT-WAZALENDO tumejifunza kutoka kwa Maalim Seif na daima hatutochoka, hatutayumba wala kutoka kwenye mstari wa kupambania mabadiliko ya dhati. Maalim SEIF ni kitabu, Shukrani kwa Viongozi wetu wa chama kwa kukipokea kitabu hiki, Vijana tumeanza kufungua kurasa zake na kukisoma, hakika kwa haya yaliyomo kwenye kitabu hiki, kizazi chetu kinaendakuimarika.
Ndugu Wanahabari, Ujio wa viongozi hawa waandamizi wa CUF umechagiza mamilion ya Watanzania kujiungana chama chetu. Ngome yaVijana ACT-WAZALENDO leo hii tunawapokea rasmi waliokuwa viongozi wa kitaifa wa Baraza la Vijana CUF (JUVICUF) ambao wameamua kuungana nasi kuipigania Tanzania mpya.

Tunachukua nafasi hii kuwakaribisha rasmi na kwa pamoja tutaendelea kusoma kitabu kiitwacho Maalim Seif tukiwa ACT-WAZALENDO. Tunawapongeza kwa uamuzi wenu sahihi, chamsingi kwapamoja tukumbuke maneno ya Mzee wetu Maalim seif aliyoyatoa juzi baada ya kukabidhiwa kadi kuwa TUTACHOKOZWA SANA NA TUSIKUBALI KUCHOKOZEKA .Kwa pamoja tunasema HATUTACHOKOZEKA . Karibuni ndugu zetu tuweze kujenga Ngome imara y… Read more

Share: