Habari

TAMWA WASHAURIWA KUENDELEA NA MRADI WA KUKUZA UWAJIBIKAJI ZANZIBAR

Daktari dhamana wa Wilaya ya Kati Unguja Bi Tatu Ali Amour akizungumzia maendeleo ya wananchi yaliyopatikana kutokana na mradi wa PAZA

Imeandikwa na Salmin Juma, Zanzibar
salminjsalmin@gmail.com
0772997018

Viongozi mbalimbali wa halmshauri ya wilaya ya kati kisiwani Unguja wameupongeza mradi wa kukuza uwajibikaji Zanzibar (Promoting Accountability of Zanzibar – PAZA) kuamsha ari kwa wananchi kupigia mbio changamoto zinazowakabili hali inayowafanya hata wao wazidishe bidii katika kutatua changamoto hizo.

Wakizungumza na waandishi wa habari waliyofika afisini hapo kwa lengo la kutaka kujua namna gani wananchi wamekua na mwamko wa wakifika kwao kupeleka kero zinazo wakabili, walisema hivi sasa ni tofauti na zamani kwani ingia toka za wananchi zimekua nyingi na wengi miongoni mwao wanakwenda kupeleka kero zao.

Daktari dhamana wilaya ya kati Tatu Tatu Ali Amour alisema, awali wananchi walikua na dhana yakua dawa hakuna tu na walikua wakilalamika sana, lakini walipoamua kutaka kujua kiundani wali waeleza kuwa, kuna aina ya dawa huja kwa awamu au kipindi maalum, hivyo walifahamu na hivi sasa malalamiko hayo yamepungua.

“mradi ndio uliyosaidia, mana walitaka kujua kwakina, tofauti na hali ilivyokua awali, tunahitaji mradi uendelee”alisema daktari huyo.

Alifahamisha, wamekua wakipokea malalamiko mengi kuhusiana na uhaba wa madaktari katika vituo vya afya pamoja na uhaba wa vyoo, jambo ambalo wamewafahamisha vizuri na wanaendelea kutatua changamoto hizo siku hadi siku.

Afisa elimu na mafunzo ya amali wilaya ya kati Makame Haji Steni alisema, muda mrefu watu walishindwa kujua majukumu yanayo wawajibikia na wengine kukosa haki zao za msingi lakini sasa wameamka na wamekua na ufatiliaji katika haki hizo.

“wanakuja wananchi wengi , wengine wanalalamikia mabati kuoza katika baadhi ya mabanda ya skuli, uhaba wa vyoo na madarasa ya kusomeshea, tunayapokea malalamiko hayo na kuyafanyia kazi” alisema Steni.

Kwa upande wake Engineer Ali Abdu Ali ambae ni afisa wa Maji wilaya hiyo alikiri kuwa PAZA umekuja kuleta mageuzi makubwa kwa wananchi na hata watendaji serikali juu ya kujitambua.
Alisema “ tunapokea wananchi tofauti wanaotaka ufafanuzi wa jambo au kuungiwa huduma ya maji, pia kuna shehia huduma haijafika vizuri kama vile kijibwe mtu , Mpapa na kwengineko na wameshaanza kudai , tupo katika kuyashuhulikia maeneo haya kuona huduma ya maji inapatikana kama kawaida” alisema Engineer Ali

Engineer Ali, alisema mradi wa PAZA unastahili kuendelea ili wananchi na watendaji kila mmoja azidi kujua wajibu wake katika nchi.

Mradi wa PAZA ulianza Novemba 2017 na unatarajiwa kumalizika Febuari 2019 mradi ambao unatekelezwa katika wilaya tatu za nguja (wilaya ya kaskazini A, wilaya ya kati na wilaya ya kusini ) na Pemba pia upo katika wilaya tatu ( Wilaya ya chakechake, wilaya ya Wete na wilaya na Micheweni)

Mradi unasimamiwa na kutekelezwa na chama cha waandishi wa habari wanawake Tanzaniab-Zanzibar – TAMWA, Jumuiya ya waandishi wa habari za Maendeleo Zanzibar – WAHAMAZA pamoja na NGENARECO kisiwani Pemba.

Na moja ya lengo la mradi huo ni kuamsha uwajibikaji kwa watendaji wa serikali na hata wasio wa serikali pamoja na kuwafanya wananchi wawe na uthubutu wa kudai haki zao kama vile, haki ya kupata huduma ya maji safi na salama, haki ya kupata huduma za afya, umeme,mawasiliano na nyenginezo.

PembaToday

Share: