Habari

Tanganyika kuivuruga CUF, lengo lake ni kuimaliza Znz:

Lile zimwi la Tanganyika kuonekana “inaionea” Zanzibar sasa inapata sura mpya,ni wazi kwamba lipumba anatumika na Taasisi za Tanganyika ili kukandamiza Zanzibar

Kila mtu anafahamu kuwa Cuf ndio chama kikubwa zaidi hata kuliko ccm  znz, lakini uanpotumia mbinu chafu kujaribu kukiua basi ni hatari kwa amani ya znz.

Taasisi za Tanganyika ndizo zinatumika kuikandamiza CUF kwa kuwa tu ina mizizi thabiti Zanzibar.

Taasisi zinazoonekana kutumika ni Ofisi ya Msajili wa Vyama ambayo tangu ianzishwe haijawahi kuongozwa na mzanzibari achilia mbali hata kuwa na Msaidizi wa msajili kutoka Zanzibar

Taasisi nyingine zinazotumika ni mahakama,mahakama kwa makusudi wameamua kuzichelewesha kwa makusudi kesi zinazohusu chama hicho japo mahakama ina majaji wengi na muda wa kutosha

Bunge la jamhuri ya muungano limeacha kazi ya kuisimamia serikali na kuwa mshirika wa serikali katika kuikandamiza Zanzibar,ikumbukwe spika na naibu wake wote ni watanganyika

Pia ofisi ya RITA ni taasisi ya Tanganyika isiyo na ushiriki wa Zanzibar lakini inataka kuamua mambo yanayoathiri taasisi zinazovuka chumbe

Hii hali inaibua hisia Kali za kitaifa na utaifa wa wazanzibar,wazanzibari wanaikumbuka Zanzibar yao,laiti wangekuwa huru wasingekuwa wananyanyasika hivi kwa makucha ya taasisi hizi

Kuna visiwa vidogo kama Comoro,wanaishi raha mustarehe hawajachomwa na kucha za nchi yeyote

Zanzibar imeanza kupata ustaarabu na kujitawala wakati Tanganyika ni mapori tu,hawajui lolotZanzibar ilikuwa Dubai ya Afrika Mashariki kwa karne na karne,leo inapondwa pondwa,wazanzibari sasa inabidi waisimamie Zanzibar kabla Zanzibar haijawa dhoofu sana kuwatetea wazanzibari

 

Share: