Habari

TANGANYIKA SASA ZAMU YENU.

Bila kutafuta namna ya kutafuna maneno kwa kuhofia au kupenda leo nimeona iko haja ya kuwa fahamisha wanaoitwa ndugu zetu iwe wa damu, kweli au kisiasa tu, ni vema sasa Watanganyika wakaelewa kuwa sisi ndugu zao wa visiwani tunaoaminishwa kuwa tumehusiana japo kuwa uhusiano huo hauwazuwii wao kututawala kwa mabavu na sisi kujipendekeza kwa kiu ya kuto kukoma kutawaliwa bila huruma huku nguvu za vyombo vya dola vikitumika kuisidikiza na kuisimika demokrasia bila ridhaa ya wahusika walio wengi,kama sio mtu mweusi tena mpinduzi na sio chotara au Muarabu kabisa haya yanayo tendeka kwetu na yanayo kuja Tanganyika huwezi kuyaelewa wala kuyapa baraka zako hata uwe na elimu ya shahada ya mwisho hiyo haitokusaidia kufikiri labda kukupa ajira pekee katika moja ya idara,mashirika na wizara za mapinduzi iwe katika chama au sirikali.

Tanganyika wakitaka wasitake na wao tayari wamesha pata kiongozi kama wale tulio wazowea huku kwetu ambao siku zote hawa heshimu maamuzi ya raia au wananchi,ni vema nikawa mkweli viongozi wetu hao au hawa hawana sababu ya kuheshimu chochote kutoka kwa waungwana sisi kwa sababu ikiwa hatukuwachagua na wanajua kuwa wamewekwa na kujiweka kwa nguvu za mitutu waliyo washikisha wajukuu zao sasa wana deni gani kwetu? Mtawala mpya wa Tanganyika Bwana au Chifu Magufuli tangu aingie katika Usultani ameshindwa kujizuwia kutawala kwa kutumia “MDOMO” wake mtupu, katiba na sheria hakuwahi kuzisikia yeye amejikita katika kutoa amri pekee tena nyingi za ovyo “decree” kila kinacho toka mdomoni mwake ndio sheria hata wanao tawaliwa wamefika kukufuru na kudai kinatoka kwa Mungu, na Mtawala huyu ameletwa na Muumba huyo huyo,sasa la kujiuliza wale kina Mwinyi,Nyerere,Kikwete na Mkapa waliletwa na CCM peke yake? au shetani alihusika na ujio huo?

Huku ni kuchangayikiwa mimi sithubutu kushtuka na kauli za aina hii kwa sababu Watanganyika juu ya kuwa ni weledi wa kutuzulumu na kututawala kwa zaidi ya miaka hamsini lakini viumbe hawa wana kasoro nyingi za kibinaadamu kama tulizo nazo sisi,huyu Magufuli hakuwa chaguo lao wengi walimtaka Lowassa,Membe na Amina katika halmashauri kuu ya chama chetu lakini baada ya mchezo kama ule wa karata wa mzungu kalala wapi, wote wakajikuta wamaimba nyimbo za kisukuma bila kutaka sasa wanatakiwa wacheze na ngoma za asili,kimila za kabila hilo hilo wameanza kugoma na kumlaani Kiongozi huyu anae wafagilisha ovyo kila jumamosi kwa nguvu, sasa nani hapa alaumiwe kwa mtukufu huyu mlie dai kaletwa na YESU.

Mtukufu mtawala wa Tangayika bila hofu wala woga ametangaza kuvipiga maraufuku vyama vya siasa kuacha kufanya kazi hiyo eti kwa kuwa ana hitaji nafasi ya kuwaletea maendeleo, na baada ya miaka mitano ndio apimwe kama anafaa au hafai, la kushangaza hapa nani kampa madaraka makubwa kama haya ya kubadili katiba ya nchi,kauli yake sio sheria wala haiwezi kuwa hivyo katika nchi yoyote yenye watu wenye akili timamu, ni lazima Watanganyika wawe wanaugua maradhi yoyote labda “amnisia”/ kusahau ovyo ovyo, ndio waruhusu amri kama hizi za kipumbavu kutukika,nimeziita za kipumbavu kwa sababu sina neno jingine sahihi,lakini pia ni lazima mimi kama Mzanzibari au Mtanzania ninae amini haki,umoja na usawa katika Muungano huu kuwatakia kila wanalo stahiki/ adhabu Watanganyika katika kipindi hiki cha utawala wa mtukufu wao, kwa sababu wao ndio kisa au msiba wa uhuru na maisha yetu.

Uungwana wangu haunizuwii kudai kisasi hasa kwa kuwa hata dini yangu imetowa baraka zake katika hili.Watanganyika mmetutesa na manaendelea kututesa kila kukicha kwa kusaidiana na hawa waislamu wenzetu hapa waliopo katika serekali yenu, sasa na nyie zamu yenu kuonja madhila ya kutawaliwa na watu au mtu mnae mjua kuwa mwenzenu lakini kumbe ni adui yenu na ataendelea kuwa hivyo siku zote mpaka pale mtakapo itafuta dawa ya kukabiliana nae.

Niliwahi kusema huko nyuma kuwa Zanzibar inaigharimu Tanganyika siku zote,kuitawala haijawahi kuwa tatizo kwa Tanganyika, tatizo ni kiasi gani Tanganyika itaelewa na kufahamu kuwa gharama wanayo ipata siku zote kwa kuikumbatia Zanzibar kwa mabavu itaimaliza kwa kuisambaratisha Tanganyika na mwisho wake Zanzibar itakuwa huru na Tanganyika itabakia vipande vipande, sasa kwa kasi ya Mtawala wenu bwana hapa kazi tu, huyu aliebatizwa jina la dikteta uchwara ambalo kwa kweli Tundu Lissu hakukosea kwa kuwa Magufuli hawezi kuwa Kagame kama vile Iddi Amini hakuweza kuwa Hitler, Tanganyika endeleeni kuitawala zanzibar lakini mkumbuke kuwa South Sudan inawapigia hodi.

Nawashukuru WAZANZIBARI WOTE/ NA kuwasalimia Watanganyika.

Share: