Habari

TANGAZO: Mkutano Mkuu wa Zanzibar Welfare Association (ZAWA)

1. Utangulizi

Zanzibar Welafare Association (ZAWA) ni jumuiya ya Wazanzibar wanaoishi nchini Uingereza kwa madhumuni ya kujenga jamii na uhusiano kwa Wazanzibar wote wanaoishi nje ya Zanzibar. ZAWA ilianzishwa May 1992, chini ya uasisi wa Marehemu Prof Mohammed Abdulrahman Babu.

2. Lengo na Madhumuni

Lengo na madhumuni ya jumuiya hii ni pamoja na:

* Kulinda na kuendeleza mila, utamaduni na desturi za Kizanzibar wakati wako ugenini.
* Kusaidia kuepukana na umasikini miongoni mwa Wazanzibar na wanachama wengine wanoishi UK, na kule nyumbani.
* Kutoa msaada kwa Wazanzibar na wanachama wanaoishi UK kujiendeleza kielimu.
* Kuwahamasisha Wazanzibar na wanachama juu ya afya bora
* Kutayarisha na kusimamia mikutano, maonyesho, semina kwa ajili ya kuwajuvya Wazanzibar na wanachama hali halisi ya maendeleo ya kiuchumi, kijamii, na kiutamaduni ya nchi yetu – Zanzibar.
* /kushirikiana na jumuiya nyengine zenye lengo na madhumuni kama haya ndani ya UK au penginepo.

3. Wanachama

Wanachama wa Jumiya wapo wa aina mbili; wanachama miongoni mwa Wazanzibar waliomba uwanachama na wanachama kutoka nchi nyengine. Wanachama kutoka nchi nyengine kwa mujibu wa katiba hawana nafasi ya haki ya kuchagua au kuchaguliwa kushika nafasi za uongozi. Uanachama unapatikana kwa kupeleka maombi rasmi, na kamati kutathmini na kutoa uamuzi wake.

4. Baadhi ya shughuli za ZAWA

Jumuiya imekuwa ikifanya shughuli nyingi ili kufikia lengo lake. Miongoni mwa mambo jumuiya iliyowahi kujishughulisha ni pamoja na:

* kusaidia misaada mbalimbali kwa wananchi wa Zanzibar, hasa katika vipindi vya majanga, ikiwemo mafuriko, ukame, kipindupindu, nk
* Kufanya mikutano ya wanachama kutoa mafunzo ya ufya, uhalifu, madawa ya kulevya, kupambana na ukimwi, nk.
* Kuanzisha madrasa za kusomesha Qurani kwa watoto wa Kizanzibr na nchi nyengine.
* Kutoa ushauri kwa serikali ikiwa ni pamoja na kukutana na viongozi mbalimbali wa vyama na serikali.

5. Mkutano Mkuu wa Mwaka

ZAWA imekusudia kufanya Mkutano Mkuu wake wa mwaka Siku ya Jumatatu, 7 May 2018 kuanzia saa 10:30AM hadi 14:30.
Mkutano utafanyika ukumbi wa: Ripple Centre,
121-125 Ripple Road
Barking, IG11 7FN

Katika mkutano mkuu kutawasilishwa report za utendeaji kwa mwaka 2017/18, report ya fedha (mapato, matumizi, na makadirio ya mwaka ujao) pamoja na uchaguzi mkuu.

6. Uchaguzi Mkuu

Kutafanyika uchaguzi mkuu wa viongozi watakaoitumikia ZAWA kwa muhula wa miaka miwili ijayo. Nachukuwa fursa kuwatangazia nafasi za uongozi wa ZAWA kwa kila mwenye shauku ya kuomba na kuiongoza Jumuiya. Nafasi hizo ni:
* MWENYEKITI
* MAKAMO MWENYEKITI
* KATIBU
* NAIBU KATIBU
* MSHIKA FEDHA
* WAJUMBE (NAFASI 9)

Fomu kwa watakaopenda kugombania bonyeza hapa upakue

Siku ya mwisho kupokea maombi ya uongozi ni 3 May 2018.

Kwa maelezo zaidi tafadhali usiache kuwasiliana nami kupitia number hii 07393225208

Zanzibar Welfare Association (ZAWA) is a Charity Organisation, Registered Charity No: 1145891

Tagsslider
Share: