Habari

Tanzania ina Democrasia??.

Assalamu aleikhum Warahmatullah Wabarakatuh ndugu Wazanzibari  na Watanganyika wa Ndani na nje ya Visiwa vyetu adhimu. Bila yakupoteza muda wangu na wa wasomaji napenda nieke wazi kwamba:

  1. woga ulioonyeshwa na viongozi wa dini Tanganyika ndio ilioipeleka Nchi ya Tanganyika kuvamia Zanzibar kijeshi  26 October 2015 na kuwadhulumu Wazanzibari haki yao ya kikatiba ambayo walimchagua maalim Sefu Sharifu na chama cha CUF kuongoza Nchi ya Visiwa vya Zanzibar katika kipindi cha miaka 5 ambayo inamalizika baada ya miezi 11 ijayo.

Ingekuwa siku ya october 26 2015 viongozi wa dini zote walisimama imara na kukemea hata kwa maandamano ushenzi uliofanywa na Jakaya Kikwete na CCm wenzake Tanganyika. Basi naamini Nchi ya Tanzania isingefikia hapa tulipo leo. Yaani ya uvunjaji wa Katiba, ufutaji wa vyama vya siasa na kuvigombanisha, utekwaji kiholela wa  wananchi wasio na hatia nakuuliwa ovyo ovyo au kushambuliwa kwa risasi na  ubakwaji wa viongozi wa vyama vya siasa na kuharibiwa mali zao au kubandikizwa kesi zisizo muelekeo.

Ndugu wasomaji munaelewa wazi kwamba juzi Magufuli aliwaita viongozi wa dini mbali mbali Ikulu na kuzungumza nao masuali mbali mbali ya kisiasa, kijamii, kiuchumi pamoja na democrasia. Kilichonisikitisha sana nikuona viongozi wachache sana wa dini hasa ya (Kikristo) ndio ambao walisimama na kutoa maoni yao au kuuliza masuali mbali mbali yaliokuwa hayakugusa kabisa kiini cha matatizo na khofu dhidi ya Wananchi.

Viongozi hao walishindwa au waliogopa kumwambia Magufuli ukweli kwamba Tanganyika na Zanzibar haina democrasia na kumtolea mifano ya matokeo mbali mbali yalio tokea au yanayoendelea kutendeka kila siku. Na kilichonitapisha zaidi nikuona viongozi wa kiislamu wao walikuwa waki kenua Mchele wa Meno tuu.

Ukweli mkutano ule ulikuwa wa Kisanii ya aina yake na nimewashusha thamani viongozi wote walio hudhuria kikao kile cha Magufuli.

Ndugu wasomaji yalipotokea yale ya 28 october 2015 viongozi hawa hawa wanaoitwa wa Kiroho walikaa kimya na kufurahia sana sakata la Zanzibar. Wengine walifika mbali nakutaka waone damu za Wazanzibari zinamwagika tena. Lakini Mungu hakusimama na wao. Isipokuwa sasa anawaonyesha yale yaliokuwa yakifanyika Visiwani Zanzibar katika miaka takriban 54 sasa; basi sasa yanatokea katika Mikoa yao ya Tanganyika. Na hata bado kuna mengi na mabaya makubwa ambayo CCM wamedhamiria kuyafanya.

Ndugu wasomaji nakumbuka viongozi wa CUF hasa maalim Sefu alikuwa akisema mara nyingi… Namnukuu… ” Uvunjaji wa Katiba ya Zanzibar uliofanyika 25.Oct. 2015 na kupinduwa matokeo halali ya Uchaguzi ni haramu na inapaswa kila Mtanzania anaependa kuiona amani ya nchi hii basi asimame na Wazanzibari kudai haki yao kihalali… Kwani tukilipuuza hili kuna mabaya mengi na mambo ya kutisha yatafanywa katika Nchi zetu mbili…” Mwisho wa Kunukuu..

Katika kipindi cha Magufuli tayari kumeshafanyika mengi mabaya na mengine yanakuja. Yet again religious leaders from Tanganyika they have eyes but they can not see it. they have ejers but they can not hear it. Inna lilah Waina ilaihi Rajiun.

 

 

 

Share: