Habari

TANZANIA KUWA MWENYEJI WA MAZOEZI YA KIJESHI,NCHI ZA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI.

TANZANIA KUWA MWENYEJI WA MAZOEZI YA KIJESHI,NCHI ZA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI.

Na Fatma Ally

Tanzania Kupitia Jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) inatarajia kuwa Mwenyeji Wa Mazoezi Ya kijeshi yanayotarajia kufanyika Novemba 5 hadi 21 mkoani Tanga.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam mkuu wa operesheni na mafunzo Jeshini Major Jenerali Alfred F Kapinga amesema lengo la mazoezi hayo yatakayohusisha vikosi vya ulinzi ni kujenga uwezo wa majeshi katika kukabiliana na changamoto mbalimbali za kiulinzi ikiwemo ugaidi na uharamia wa bahari sambamba na kubadilishana uzoefu kwa kujenga
mahusiano ya kijeshi.

“zoezi hilo ambalo tumelipa jina la ushirikiano imara ni zoezi la medani yaann(FTX) litafanyika kwa wilaya za Tanga mjini na Muheza kuanzia Tarehe 05 novembemba hadi 21 Novemba 2018″amesema Meja jenerali Kapinga.

Hata hivyo, ameongeza kuwa katika mazoezi hayo pia kutakuwa na kazi za kusaidia jamii kama vile ujenzi wa madarasa, ofisi za walimu pamoja na vyoo katika Shule ya msingi machemba Iliyopo wilayani Muheza Sambamba na utoaji wa huduma za tiba kwa wananchi huku akiwataka wananchi kujitokeza kwa wingi katika zoezi hilo.

Aidha ameongeza kuwa majeshi Ya ulinzi na usalama ya nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki Yatakayoshiriki Mazoezi hayo ni pamoja na majeshi Ya nchi Kavu,majini Na Majeshi ya anga ambapo wanajeshi zaidi ya 1500 kutoka katika nchi za Tanzania,Kenya,Uganda,Burundi na Rwanda wanatarajia kushiriki.

Tagsslider
Share: