Habari

TANZANIA YAIPIGA MWELEKA ZANZIBAR UMOJA WA MATAIFA KUHUSU ENEO LA BAHARI YA HINDI.

Nimasikitiko mengine tena kwa Wazanzibar walio wengi, walio masikini, wanyonge na wenye kudharauliwa na Watanganyika katika kila siku zinavyokwenda mbele.

Tumeshughudia kwa mara nyengine tena wenzetu tunaowaita ndugu wa damu Watanganyika wanavyohangaika kila pembe ya dunia kujiletea maendeleo kwa kupitia kivuli cha Muungano wa Tanzania na kuwaacha Wazanzibar wakiwa hawajui wapi pa kuanzia na kukamatia.

Tulitegemea katika suala zima la utaratib Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kupitia Baraza la Mawaziri au hata Baraza la Wawakilishi wangeshirikishwa kwa njia moja au nyengine, lakini ni masikitiko makubwa tena yasiokuwa na kuambiwa pole ndugu zetu W3atanganyika wametuendea kinyume kwa maslahi yao ya kimaendeleo

Lengo kuu la Serikali ya Tanzania kupeleka maombi Umoja wa Mataifa ni kwaajili ya kupanua eneo la bahari na kuhakikisha raslimali zote zilizokuwemo katika eneo hilo tunalolizungumzia linakuwa katika umiliki wa Tanzania/Tanganyika.

Ndugu zetu teyari wanajua kwamba eneo la bahari ambalo linapakana na visiwa vya Zanzibar kuna kiwango kikubwa cha mafuta na gas. Kwa utafiti uliofanyika na wakaona kwamba ikiwa hawatofanya maombi katika umoja wa mataifa kuna uwezekano mkubwa sana hayo mafuta na gas wakaikosa kama ambavyo Mh Samuel Sitta alivyosema hatowezekana kwa Zanzibar kuchimba mafuta na gas bila ya Tanzania bara kushirikishwa.

Kwahiyo teyari wamepata ufumbuzi wa kuweza kuyamiliki mafuta na gas katika mwambao wa Zanzibar kwa kupitia maombi rasmi yaliofikishwa Umoja wa Mataifa.

Tunakumbuka Baraza la Wawakilishi liliitaka Serikali ya Zanzibar iunde chombo cha kusimamia uchimbaji wa mafuta…Zanzibar Petroleum Corporation(ZPC)a lakini Mh Shamuhuna mwenye zamana ya Wizara yake ya maji na madini ameshindwa kuunda hilo shirika na matokeo yake tumeona wajumbe walioshiriki kupeleka maombi Umoja wa Mataifa miongoni mwao ni Manager mkuu wa Tanzania Petroleum Corporation.

Leo Mh Shamuhuna anatwambia kwamba hakuwa na muda wa kutosha kuhudhuria kupelekwa kwa maombi UN..na akatuma muwakilishi wake…Jee hii kweli inaingia akili?

Watanganyika kwa ufupi hawalidhamini na kulitambua Baraza la Wawakilishi la Zanzibar ndio maana wanafanya maamuzi vile ambavyo wanataka au wanapenda. Kama ingelikuwa  wanalitambua Baraza la wawakilishi wasingefikia hatua waliyofikia leo….Nindugu zetu wa damu lakini hapa inasikitisha sana kwa matendo yanayofanywa na ndugu zetu.

Inawezekana Serikali ya Tanzania Bara imeijuulisha Serikali ya GNU kuhusu mategemeo ya kupeleka maombi Umoja wa Mataifa, lakini kwa uzembe na kutowajibika na kufuatwa taratibu ndio leo tunasikia kauli mbali mbali za Mh Shamuhuna kwamba hakuwa na muda wa kutosha kufuatilia hili suala nyeti.

Jee ikiwa UN itakubali ombi lililowasilishwa na Tanzania na Wazanzibar wakakataa hatua gani zitachukuliwa na Wazanzibar?

Tumeona kwamba Baraza la Wawakilishi  chombo cha kutunga Sheria Zanzibar hakina sauti, hakina mamlaka yoyote nje ya Zanzibar, baraza na sheria zake zinazopitishwa hazitambuliwi na Tanzania bara..Jee hatua hii tutafika?

Kwanini wawakilishi wasiwe na sauti moja kupinga kwa nguvu zote kudharauliwa na Ndugu zetu wa Tanganyika katika kila kinachoamuliwa na Wazanzibar.

Jee viongozi wa GNU muko wapi? haya yanayotokea hamuyaoni? Sheria ya Mwaka 2010 iliyompa Rais wa Zanzibar mamlaka ya kuigawa Zanzibar bila ya kumshirikisha Rais wa Jamhuri ya Tanzania hapa hii sheria haitumiki.

Kwanini Rais wa Jamhuri wa Tanzania anakuwa na mamlaka ya kuomba eneo jengine hata ndani ya mipaka ya Zanzibar? ambapo sheria imeshatamka wazi kwamba Rais wa Tanzania hana mamlaka ya kuigawa Zanzibar au kuiongezea ukubwa kwa kupitia chombo chochote kile .

Kwanini Zanzibar isiwasilishe maombi UN kwa kuongezewa eneo la bahari…Wanganyika watumie mgongo wa MUUNGANO kuomba eneo zaidi la kuchimba mafuta na gas…? Wazanzibar wamelala….au hakuna wataalamu wenye elimu kuandika maombi….tunasikitika sana wenzetu ndugu zetu wametupiga kikumbo tena mchana sio usiku.

Nimategemeo yetu na vizazi vyetu kudumisha umoja na undugu na ujirani mwema na ndugu zetu wa Tanganyika lakini kwa hali hii sijui kama tutafika.

 

Share: