Habari

Tuangalie nchi zilizokuwa na muungano na vipi zilipata uhuru wake

Jamuhuri ya Watu wa Zanzibar iliungano na Jamuhuri ya Tanganyika mnamo April 1964 na kuunda Jamuhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, ambayo baadae ilijulikana kwa jina la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. Miaka 54 sasa imepita tokea muungano huu na bado unaendelea ukiwa haujavunjika. Kumekuwa na malalamiko ambayo yamekuwa yakitolewa na moja kati ya nchi zilizounda muungano. Leo tuangalie miungano ya nchi nyengine na kile kilichopelekea kuvunjika kwake. Sababu kuu ya kuvunjika kwa muungano ni pale nchi moja inapoona haitendewi vyema na washirika wa muungano hivyo kutaka kujitowa.

EAST TIMOR (Timor-Leste) na INDONESIA

East Timor yenye watu 1,167,242 kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2015, ni visiwa vilivyoko Kusini Mashariki ya Asia baina ya Indonesia na Australia, kwenye karne 16th vilitawaliwa na Wareno hadi 28 November 1975 ilipopata Uhuru kutoka kwa Wareno. Siku tisa tu baadae ilivamiwa na kukaliwa na Indonesia na kutangazwa kuwa jimbo la 27 la Indonesia. Kukaliwa huku kulipelekea visiwa hivi kugubikwa na wimbi la ghasia na machafuko. Takwimu za Kamati ya Maridhiano zinaonyesha kwa uchache watu 102,800 walipoteza maisha yao kwa machafuko kati ya kipindi cha 1974–1999. Hali iliyotokana na ghasia na machafuko baina ya Wanaotaka kujitenga na Majeshi ya Indonesia. Wapiganaji wa msituni waliongoza mapambano ya kuiondowa Indonesia katika kipindi hicho.

Mauwaji ya kimbali ya mwaka 1991 ilikuwa chanzo kuelekea kupata uhuru wake kuliko changiwa na wanaharaki wa East Timor waliokulia Ureno, Australia na nchi nyengine za Magharibi. Mwaka 1999, kufuatia United Nations (UN) kusimamia kupatikaa uhuru wake, Indonesia kwa hiari yake ilikubali kuiachia East Timor. UN iliingia makubaliano na Indonesia pamoja na Ureno kuitisha kura ya maoni iliyosimamiwa na UN. East Timor ikawa nchi ya mwazo kuwa huru katika karne hii ya 21 tarehe 20 May 2002, pale ilipotambulika na kujiunga na Umoja wa Mataifa (UN).

ERITREA na ETHIOPIA

Kufuatia uamuzi wa UN General Assembly mwaka 1952, Eritrea ilitakiwa kuwa huru huku ikiwa na utawala na vyombo vya kisheria, bendera yake, na kuwa na udhibiti wa mambo yake yote ya ndani ikiwa ni pamoja na polisi, ushuru, na utawala. Pia ilitakiwa kuunda muungano wa shirikisho na Ethiopia kwa mambo ya; biashara, mambo ya nje, ulinzi, fedha, na usafiri. Muungano wao ulikuwa kwa kipindi cha miaka 10 tu. Ilipofika mwaka 1962 ukiwa ndio mwisho wa makubaliano, Ethiopia ilivunja bunge la Eritrea, na rasmi kujimilikisha kuwa moja kati ya majimbo yake. Wa-Eritrea ambao tokea 1942 wakipigania uhuru hawakufurahishwa na jambo hili nakuanza kujipanga na kuunda kundi la ukombozi kupambana na Ethiopia.

Kundi hili liliundwa na Wa-Eritirea wanafunzi, professionals, na wataalamu wengine. Walijikita zaidi kupinga sera za kuifanya nchi moja chini ya utawala wa Kifalme wa Ethiopia. Mwaka 1961, the Eritrean People Liberation Front (EPLF), chini ya uongozi wa Hamid Idris Awate, ulianzisha utumiaji nguvu na silaha kupigania uhuru. Mwaka 1962, Haile Selassie kivyakevyake alilivunja Bunge la Eritirea na kuifanya jimbo chini ya himaya yake. Vita vya kupigania uhuru vilendelea kwa kipindi cha miaka 30 mfululizo hadi ilipofika mwaka 1991 pale Eritrean People’s Liberation Front (EPLF) walipofanikiwa kuyashinda majeshi ya Ethiopia. Gharama ya vifo vya watu zaidi ya 70,000 kwa pande zote.

Kufuatia UN kusimamia kura ya maoni Eritrea, ambapo wananchi kwa wingi walipiga kura kutaka uhuru, ndipo Eritrea ilijitangazia uhuru wake na kupata utabulisho wa kimataifa mwaka 1993. Eritrea ni mwanachama wa United Nations, African Union, na observing member of the Arab League.

SOUTH SUDAN na SUDAN

South Sudan ilikuwa ni eneo katika nchi ya Sudan. Kufuatia vita vya mwanzo vya wenyewe kwa wenyewe vilivyokuwa vikiendelea, Sudan Kusini ilijitangazia mamla yake kijimbio mnamo mwaka 1972 hadi mwaka 1983. Vita vya pili vya wenyewe kwa wenyewe vya Sudan ghafla vilichomoza tena ambavyo vilidumu kwa muda mrefu mzaidi hadi mwaka 2005, vilimalizika kwa kufugiana mkataba amaani.

Sudan became an independent state on 9 July 2011, following a referendum that passed with 98.83% of the vote. South Sudan yenye wakaazi milioni 12 sasa hivi ni mwanachama wa United Nations, African Union, na East African Community.

Share: