Habari

Tumkumbuke mmoja kati ya Wapenzi wangu, Waride Bakar Jabu

KATIBU wa kamati maalum ya NEC, Idara ya Itikadi na Uenezi CCM Zanzibar, Catherine Peter Nao (kushoto),akikabidhiwa ofisi na taarifa ya secretarieti ya NEC ya Idara ya Itikadi na Uenezi CCM Zanzibar kutoka kwa aliyekuwa katibu wa Idara hiyo aliyemaliza muda wake Waride Bakari Jabu, hafla hiyo imefanyika Kisiwandui.

Mzee Kondo mara nyingi alikuwa akipenda ku-quote miongoni mwa misamiani ya Bi Waride Bakar Jabu.

Leo imenijia machoni sura ya Bi Waride Bakar Jabu, mmoja wa wafanyakazi wa Kisiwandui. Macho yangu yamejenga haiba na mvuto wa Bi Waride vile macho yake yanapopepesa. Sauti ya Bi Waride pia huwa naikumbukia kwa vile vimbawanga na mipasho yake. Mwanasiasa kijana, mwanamke mrembo aliyelimudu jukwaa, ambaye nyota yake “iling’ara ghafla ikazimika”.

Namkumbuka Bi Waride wakati yupo nyumbani kwao Mbweni alipokuwa akiishi na familia yake kwenye jumba la kifakhari huku kazi yao kubwa ikiwa kilimo cha mbogamboga. Enzi zile nilikuwa nikiishi Mbweni pia. Nyumba yao ilikuwa pembezoni mwa barabara, ilikuwa ndio njia yetu, lazima mara mbili kwa siku nipite mbele ya nyumba yao. Mara ya kwanza wakati wa kwenda skuli na mara ya pili wakati wa kurudi skuli. Ukiachia mbali nyakati za kutia viringi, wakati huo Bi Waride ndio hivyo tena, ukipita mara moja watamani urudi mara nyengine ya pili.

Siku zimepita, punde Bi Waride kapanda. Mwaka 2010 alimuangusha mpinzani wake kuwania nafasi ya Ubunge jimbo la Kiembesamaki. Kwa upande wa Uwakilishi mshirika wake alikuwa Bw Mansour Yussuf Himid, ambaye alikuwa Waziri wa Maji Ujenzi Nishati na Ardhi. Kufuatia uchaguzi mkuu wa 2010 nyota ya Bi Waride iling’ara ndani ya macho yake mazuri. Upande wa mshirika wake, mara tu baada ya uchaguzi nyota ya Bw Mansour iliporomoka.

Bi Waride alichaguliwa na kushinda kiti cha Ubunge kwa kipindi cha 2010 – 2015. Baadae aliteuliwa kuwa Mbunge wa Bunge la Katiba ya Jamuhuri ya Muungano, na hapohapo akateuliwa kuwa Makamo mwenyekiti wa Kamati namba saba, chini ya Mwenyekiti Brigedia Jenerali (mstaafu) Hassan Ngwilizi. Baada ya uchaguzi wa CCM kufanyika mwaka 2012, aliteuliwa kuwa KATIBU wa Kamati Maalum ya NEC, Idara ya Itikadi na Uenezi CCM Zanzibar. Nafasi nne nzito na kubwa kuzifanya kwa pamoja.

Kwa bahati mbaya Bi Waride, vyeo vilianza kumtoka. Mwaka 2015 aliangushwa kwenye kinyang’anyiro cha kugombea tena Jimbo la Kiembesamaki nafasi ya Ubunge, pale Bw Ibrahim Raza, ndugu yake mfanyabiashara na mwanasiasa maarufu Bw Mohamed Raza (Mbunge wa Uzini), alipomgaragaza na kumtowa nje ya ulingo wa kurudi tena bungeni Dodoma. Kufuatia uchaguzi mkuu wa CCM mwaka 2017, Bi Waride pia kaanguka tena kuitumikia CCM hapo Kisiwandui, nafasi yake sasa imeshikwa na Catherine Peter Nao.

Kama mdadisi sitosita kutaka kujuwa kipi kilichomtokea Bi Waride hata aanguke vibaya katika kipindi kifupi kama hichi, licha ya mbwembwe, pozi zake, uzuri wake na personality yake machoni mwa wengi. Moja na kubwa ni hili ambalo mrithi wa nafasi yake, Bi Catherine Peter Nao aliposema; “idara yangu ina wajibu wa kutekeleza na kufanya kazi ya kuhakikisha CCM inashinda katika kila uchaguzi na kwamba ndio sehemu muhimu ya chama kuwa na mafanikio kisiasa.” Kushindwa kwa CCM katika uchaguzi wa mwaka 2015, imeonyesha kuwa Bi Waride aidha hakufahamu madhumuni ya idara yake, au uwezo wake ulikuwa mdogo kuliko majukumu ya idara yake.

Mrithi wake sasa, Bi Cathy ametaja kipaumbele chake ambacho anatarajia kuanza nacho katika utendaji wake kuwa ni kutekeleza kwa vitendo ibara ya 5 ya katiba ya chama hicho. Alisema ibara hiyo inaeleza wazi kuwa kila uchaguzi ukifika CCM inashinda katika serikali za mitaa hadi serikali kuu na kwamba kazi ya chama cha siasa ni kushinda na kushika dola. Pia, anatarajia kuendeleza mambo mema yaliyofanywa na mtangulizi wake huku akibuni mikakati mipya itakayosaidia kurahisisha utendaji wa shughuli za chama.

Binafsi ni mpenzi mkubwa wa Bi Waride, na moja kinachonifanya nimkumbuke ni kwa ile kauli yake kwa Bw Aboubakar Khamis Bakar, aliyekuwa Waziri wa Katiba na Sheria. Hadi leo nikikumbuka hotuba ya Bi Waride uso wangu hukunjuka kwa bashasha na kumtazama Bi Waride kwa angle nyengine ya jicho langu. Bi Waride alimtumia salamu Bw Aboubakar, alimwambia “Kama wanambia nina machuchu makubwa njoo unyonye…”

Natamani nimuone tena kwenye ulingo na majukwaa ya kisiasa mrembo Waride, hasa kwa menngi mazuri aliyoyafanya kwenye CCM. Bi Waride amesema katika kipindi chake cha kazi alifanya jitihada za kuhakikisha chama inamiliki vyombo vyake vya habari ikiwemo radio ya Bahari ili kurahisisha kazi ya uenezi.

Kibaya alichokifanya Bi Waride ni kuuwa KAMATI YA MARIDHIANIO. Kwenye taarifa yake alisema “Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinapenda kuuelezea na kuwajulisha wananchi na Jumuiya ya Kimataifa kuwa hakiitambui na hakina mnasaba na Kamati ya Maridhiano inayodai kuwa ina uwakilishi wa wajumbe toka vyama vya CCM na CUF hapa Zanzibar. CCM ina utaratibu na kanuni zake za kuunda kamati na si kuundiwa au kusemewa na kundi lolote. Chama Cha Mapinduzi kinaitambua Kamati ya HASSAN NASSOR MOYO kuwa ni Kamati ya mvurugano yenye malengo na madhumuni binafsi kwa tamaa na kukamilisha haja na matakwa yao. Kamati ya Maridhiano ya inayoongozwa na Moyo haitambuliwi na Kamati Malum ya NEC Zanzibar, Kamati Kuu ya CCM na wala Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC). Ni vyema toka sasa wajumbe wanaojiita ni wawakilishi wa CCM katika kamati hiyo wakaeleza wamepata wapi ruhusa au wametumwa na kiongozi gani wa juu wa CCM ili kushiriki kwenye kamati hiyo. Mwisho CCM inawajuulisha Wazanzibari na Watanzania kwa jumla kuwa haihusiki kabisa na Kamati ya maridhiano inayovishirikisha vyama vya CCM na CUF hapa Zanzibar”.

Bi Waride jipange urudi tena ulingoni na jukwaani, nina kumiss so much my love.

Tagsslider
Share: