HabariMatangazoMisaada

Tumsaidie Mwenzetu yuhali mbaya

Bi Asha Khamis, anaeonekana pichani ni mkaazi wa Pemba, ambae pia ni mama wa watoto wanne, ambao watatu katika hao ni walemavu wa akili, mabubu na hawawezi kutembea na wala hawana hisia za mahitaji ya kuenda haja kubwa au ndogo, bila ya uangalizi wa mama yao, anakabiliwa na mtihani wa kupoteza miguu yake miwili kutokana na majeraha makubwa yaliyosababishwa na ugonjwa wa kisukari.

Tayari mama huyo ameshakatwa vidole vitatu katika mguu wake mmoja na kama hatopatiwa matibabu ya haraka basi anaweza kupoteza miguu yote miwili kwa vile mguu wa pili nao unaonyesha dalili ya kuharibika. Hivi sasa mama huyo anatembea kwa kugaragara kutokana na kuathirika kwa nyayo za miguu yote miwili.

Kutokana na hali yake kuzidi kuwa mbaya zaidi, wahisani na familia yake wamempeleka Dar kwa matibabu. Kutokana na gharama za matibabu kuwa kubwa, wamelazimika kumuuguzia nyumbani kwao Kawe, ambako humpeleka na kurejesha hospitali kutokana na kukosa fedha za matibabu na gharama nyengine zikiwemo za kumlaza katika wodi maalum kwa uangalizi zaidi.

Huyu mama ni maskini na hana uwezo wa kugharamia matibabu yake. Kwa watakaoweza kuchangia chochote, namba zifuatazo zitumike kuwasilisha michango yao kwa kupitia NGO yetu ya ZAVCO ambayo inatoa huduma kwa jamii katika masuala ya Afya ya jamii na Elimu.

Wawakilishi wetu katika Diaspora ni hawa wafuatao: Ndugu Haji Jingo, kwa walioko Marekani, Bibi Sophie Msomali kwa walioko Uingereza, Bwana Hilal Hilmi kwa walioko Oman, Bwana Mohammed Ghassani kwa walioko Ujerumani, na Bibi Layla Salum (Mamaaisha) kwa walioko Sweden.

Tunatafuta wawakilishi kutoka Dubai, Canada, Belgium na Norway, ambao watasimamia michango ili kuwezesha huduma za dharura kama hizi na yenginezo katika masuala ya afya na elimu kwa kupitia taasisi yetu hii.

Kwa waliopo Tanzania, munaweza kutumia contacts hizi hapa kwa michango yenu: +255 714 870 004 Jina ni Dhamir Yakout na +255 713 187 733 Jina ni Maryam Marshed. Kwa ambao watapenda kwenda kumuona Bi Asha, wawasiliane na watu hawa: +255 776 041 420. Anaitwa bwana Khatib, huyu ndio anaemshuhulikia Bi Asha huko Kawe Dar es salaam. Mwengine ni Bi Hadia mwenye nambari +255 777 877 920. Tafadhali sambaza ujumbe huu.
Ahsanteni

Share: