Habari

TWALA ALIYAJUA NA KUYAONA HAYA AKIWA JELA.

Kama hufuatilii siasa hapa kwetu au umezaliwa Zanzibar kwa bahati mbaya tu, unaweza kudhani visiwa hivi hatujawahi kumdhuru/kumuuwa hata kunguni,lakini ukweli umejificha katika nia na roho za wale walio zaliwa na kufuatilia siasa zetu kwa makusudi.

Hapa visiwani sisi tumeizowea misiba mingi inayotukuta kwa kulazimishwa, hata unapo himizwa ukapige kura kuwa kufanya hivyo huwa unatimiza haki yako ya kikatiba, basi jaribu upige kura hiyo bila kutuuliza umpigie nani? uone lini tutakufukuza kazi,kuku bomolea nyumba,kama hatujakuteka na kukujeruhi basi tuta kuuwa kabisa, hayo yote tunafanya na bado tutakuomba ukubali kuwa wewe ni raia au mtu huru katika nchi au visiwa vilivyojaa au kufurika amani na utulivu.

Ni desturi yangu nikiwa na muda wa kuchezea baada ya kutafuta riziki hukaa nikaanza kupitia kadhia nyingi za zamani,hivi karibuni nilipata fursa tena ya kumsikiliza kwa makini al-marhum Amani Thani kwenye moja ya mkanda wake wa vidio, aliotuwekea kumbukumbu zake kabla hajatangulia katika haki.

Kwa kweli nime farijika sana sana kuona kuwa huyu mheshimiwa aliyekuwa “general secretary” wa ZNP yaani Zanzibar Nationalist Party al maaruf HIZBU,bado japo kuwa yupo kaburini lakini elimu anayotowa inaendelea kutufaa wengi tunaotaka kujua wapi tunakosea kila siku.

Marehemu Bwana Amani Thani wakati akiwa kifungoni,kwanza kwa bamkwe na baadae gerezani kinua miguu {kilimani} na baadae kinumoshi au kizimbani{langoni} katika kumbukumbu zake anasema yeye alikuwa muda mwingi wakizungumza na kupanga mengi na aliyekuwa waziri wa fedha na baadae afya wa serekali ya mzee Karume muungwana Abdulaziz Ali Khamis Twala,kwa kuwa walikuwa wakionekana wako pamoja mara nyingi wakinon’gona,jambo hili liliwakera sana wafungwa wengine wawili ambao na wao waliletwa gerezani pamoja na Twala,waheshimiwa hao walikuwa mabwana Mdungi Ussi na Jaha Ubwa.

Jaha Ubwa na Mdungi Ussi walimshangaa Twala na walimueleza kuwa kwa nini anashirikiana au yuko karibu sana na Bwana Thani,walitaka kujua kuwa yeye hajui kuwa huyu Amani Thani ni HIZBU?pia humo gerezani hamna upungufu wa wana AFRO SHIRAZI kwa nini yeye anamshiriki adui yao?

HAPA NDIPO ALIPONIKOSHA TWALA NA KUNIFANYA NIKUMBUKE HAPA TULIPO LEO SISI WAZANZIBARI.

Twala aliwashangaa kama walivyomshangaa yeye kwanza kisha,akawafahamisha kuwa nyie bado mna fikra za kuwa sisi Afro shirazi na huyu au hawa mahizbu? angalieni kama mmesahau humu au hapa TUMO JELA, na sisi sote ni wafungwa tumefungwa na hao Afro Shirazi,sasa ni wazi kuwa sisi sio Afro shirazi tena na humu sote ni wapinzani au maadui wa serekali hiyo tuliyokuwa sote tunaiongoza huko nje.

Wazanzibari sisi mpaka leo tunashindwa kuyajua au kuyaona haya aliyoyaona Bwana Twala katika miaka hiyo ya 1960s wakati akiwa jela,sisi mpaka leo mwaka 2018 bado kuna wenzetu wanadhani wao CCM na sisi sote mahizbu au maadui,wanachoshindwa kukiona au kukijua kuwa sisi sote tumo katika GEREZA LA TANGANYIKA.

Humu katika gereza hili la mkoloni tunaungua na kuumia sote,tuna jimaliza wenyewe kwa kuendelea kubaguana kivyama,kiitikadi,kikabila,kimikoa,kirangi au kidini,mtawala yaani Tanganyika anafarijika sana anapotuona sisi humu gerezani{zanzibar}bado tunakataa kuongea au kupanga chochote na Bwana Amani Thani{Maalim Seif}kwa kuwa huyu HIZBU.

Huu ni mmoja ya misiba yetu ya miaka nenda miaka rudi,siku zote nikipata nafasi hupenda kulirudia somo hili ili ndugu zangu tufahamu kuwa sisi tunataka wenyewe kutawaliwa hatujalazimishwa na mtu,huwezi kuwatawala watu kwa nguvu ikiwa hawataki,tatizo ni hawa wenzetu wanaofikiri wao bado ni Afro shirazi{ccm}halali japo kuwa wamo jela pamoja na sisi.

Hivi visiwa tuna viangamiza wanetu na wajukuu zetu hapa watakuwa kama wapo Dododa karibu kwa uchache wao,dini inaondoka taratibu,mila zimetukimbia na utamaduni wetu umebadilishwa,unapovimaliza vigezo hivi unaondoa “identity” na unapo ondoa utambulisho unakuwa umefanikiwa kuuwa Utaifa wa mtu.{nchi}

Haya yote si kitu kwa waheshimiwa wetu hawa wanaojali matumbo yao na yale ya wake zao{familia} wanadhani wako nje huru kwa kuwa wanalipwa mishahara minono na wanapanda magari ya kifahari,hawakuona haya wala vibaya kuwafungisha masheikh Tanganyika,lengo lao ni kuuwa dini,unafikiri kuna siku wataletwa mapadri hapa kuja kufungwa jela ya kinumoshi au kinua miguu,yaguju.

Sisi tutatawaliwa milele ikiwa bado hatuja soma yaliyowakuta wazee,ndugu,jamaa na wazanzibari wenzetu waliouliwa kwa makusudi ili sisi tutawaliwe vizuri,ndio maana bado mpaka leo bado tunauwana kisa uchaguzi,tatizo sio uchaguzi,tatizo  hili koloni ni la watu na sisi ni “Tanganyika subjects”someni historia yetu sana mtagundua kuwa haya yanayofanyika leo sio mageni,yameanza zamani sana lengo lililo kusudiwa tunalikaribia kila siku zikisogea.

Makosa ya uchapaji mtanisamehe sikupata muda wa kuhakiki.

Mola awalaze pema wale wote walodhulumiwa roho zao katika magereza yetu,pia atunusuru na kutupunguzia mauti/makali na sisi tulio katika gereza hili la TANGANYIKA.

Ameen.

Share: