Habari

UBAGUZI WA AJIRA ZANZIBAR, JEE NI ILANI (SERA) YA CCM ?

UBAGUZI WA AJIRA ZANZIBAR, JEE NI ILANI (SERA) YA CCM ? .

Mwaka 1964 baada ya Mapindu ya 12 January, SMZ iliwatoa Kazini Washirazi, Waarabu, na Wahindi wote ambao walikuwa na haki sawa Waafrika(watumwa) ambao ndio waliopindua serikaki iliyo chagukiwa na Wazanzibar.
Ubaguzi huo uliendelea na kushika kasi na kupaliliwa kipindi cha Komandoo Dokta Salmin Amour kwa watu wenye asili ya pemba na wapinzani wa wakihamishwa makazini na makaazi bika ya kupewa stahiki zao.

Wapinzani wa CCM waliendelea kupata tabu hadi pale nusra ilipo wafikia ya Makubaliano (maridhiano) ya Dr Amani Abeid Karume alipo amua kuzifata nyao za Babayake Marehemu Abeid Karume.

Rais Aman alimua kushiriana na Malim Seif Sharif kwa kuondisha tofauti zao na kuwaunganisha wanzanzibar kwa kurejesha umoja na upendo.

Umoja huo ulifanikiwa kudumu kwa kipindi kimoja cha serikali ya umoja wa kitaifa, leo hii madhila yamerudishwa tena awamu hii ya CCM, wazanzibar wenye asili ya Pemba na upinzani wamereshwa mwaka 1964 kwa kubaguliwa na kunyimwa fursa za ajira na kurudishwa nyuma kimaendeleo, zanzibar ili uweze kupata ajira hadi upite ukaguzi wa JSO wakishikiana na sheha,hadi upekuriwe ili utambuliwe msimamo wako,asili ya wazee wako na chama choko, ikigundulika asili yako ni pemba au ukiwa munguja na mpinzani basi huwezi kupata ajira.

Haya yanafanywa kwa nia ya kuwati adabu wapinzani na wapemba kwa kuikataa CCM na kutokuiunga mkono chama cha CCM kwenye uchaguzi uliopita 25 october 2015 , kitendo hicho kinacho fanywa na SMZ ni kinyume na utawala wa sheria na utawala bora.

Jee hii ni ilani ya CCM inavyo sema ? Kua vijana wa upinzani wafanyiwe ubaguzi, au hayaa ndio magizo kutokaa juu, ni imani yangu Dr Bashiru alieshiba philoshopy za BaBa wa taifa na ujamaa anawajibu wa kulifanyia kazi hili na kutupa majibu juu ya ilani ya ccm kua inahubiri ubaguzi au matashi ya kikundi cha wachache wasioitakiya mema zanzibar na CCM ndio wanafanya ubaguzi hu kwa wazanzibar.

Hakika baada ya dhiki faraja, Wazanzibar kwa historia yao hawajawahi kukata tamaa wala kujuta juu ya mamuzi yao, imani yangu vijana wote wenye kufikwa na madhila haya ya CCM na SMZ hawatochoka kupigania haki kwa maslahi ya zanzibar na Tanzania.

Mungu ibariki Tanzania
Mungu ibarik zanzibar
Mungu wabariki wazanzibar
Mungu wabariki wazulumiwa wote
Mungu wabariki wapigania haki na wapenda maendeleo.

Omokha.

Share: