Habari

Ufunguzi wa ilani ya CUF Zanzibar

Zanzibar. Chama cha Wananchi (CUF), Zanzibar kimezindua ilani yake inayoainisha vipaumbele 35 ambavyo kitavifanyia kazi chini ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa iwapo kitashinda Oktoba 25.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa ilani hiyo Mji Mkongwe Zanzibar,Katibu Mkuu wa chama hicho Maalim Seif Sharif Hamad alisema hiyo ndiyo dira ya miakamitano ya uongozi wake.

Maalim ambaye ndiye mgombea urais kwa tiketi ya CUF Zanzibar, alisema watarejesha mamlaka kamili ya Zanzibar kwa kuimarisha Muungano utakaozingatia misingi ya haki, usawa na heshima kwa nchi zote mbili.

Alisema kitajenga uongozi mwema kwa kuimarisha misingi ya uhuru, haki na maridhiano kwa wananchi wa Zanzibar pamoja na kulinda, kuenzi, kuendeleza, kuijenga na kuimarisha misingi yote ya umoja wa kitaifa ambayo alisema waasisi wake ni yeye na rais mstaafu, Amani Abeid Karume.

Aliahidi kupambana na rushwa, ufisadi, upendeleo, uonevu, ubaguzi na woga kwa kurekebisha nmuundo wa utawala, uwajibikaji na utendaji katika kazi na utoaji wa huduma sambamba na kupanua viwango vya elimu na uelewa wa kutosha kwa jamii.

Chanzo: Mwananchi

Tagsslider
Share: