Habari

UHARAMIA MKUBWA WAPANGWA KUFANYWA ZANZIBAR

Na Chanzo cha kuaminika

Zanzibar hasa kisiwa cha Unguja kunaandaliwa mipango ya uharamia mkubwa kwa kutumia silaha za moto na miripuko yenye lengo la kujeruhi vibaya na kuuwa. Kwa mujibu wa habari zilizopatikana kutoka kwa wanausalama wasiopendezwa na mipango hiyo yenye kutokana na siasa zenye dhamira potofu mipango hiyo inapratibiwa na watu maalum wenye mahusiano ya karibu sana na dola, ndani ya serikali zote mbili, ile ya Mapinduzi ya Zanzibar na ile ya Jamhuri ya Muungano.

Baadhi ya wahusika wakuu wanaotajwa kuhusika na mpango huu ni Haji Omar Kheir, kiongozi muandamizi ndani ya serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Boniface Mwale kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mjini Maghrib. Wengine ni viongozi wa dini wakiwemo Sheikh Alhadi Mussa, Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam na Sheikh Salim maarufu kwa jina la Msomali wa Malindi Unguja. Vinara wengine wa mpango huo ni Advocate Mayugwa, RPC wa Mjini Maghrib, Hassan Nassir Ali, Mkuu wa kituo cha Polisi Mazizini, Wilaya ya Maghrib, Unguja, Bwana Amani Ibrahim Amani wa Nyamanzi na raia wa kisomali kiasi watano wanaoishi Ununio Dar es Salaam.

Sheikh Alhadi Mussa anaratibu raia wa kisomali wanaoishi Ununio Dar es Salaam na Sheikh Salim (Msomali) anaeishi Malindi Unguja. Wasomali wa Ununio watakabidhiwa mzigo wa silaha na miripuko ambao utatakiwa upelekwe Zanzibar. Mzigo huo utaingizwa Zanzibar na wasomali wa Ununio kupitia bandari bubu zilizoainishwa ambazo ni bandari ya Buyu Chukwani na bandari ya Kisakasaka. Mzee Amani Ibrahim wa Nyamanzi ataupokea mzigo huo na utakwenda kuhifadhiwa kwa Mzee Mayugwa. Wasomali waliouingiza mzigo watafikia kwa Mzee Mayugwa na baadae kuchukuliwa Sheikh Salim (Msomali) kama wenyeji wake.

Mkuu wa kituo cha polisi Mazizini na RPC wa Mkoa wa Mjini Maghrib wanatakiwa kuufahamu mpango huu kutokana na uingizwaji wa mzigo wa silaha na miripuko utafanyika katika maeneo yao ya kiulinzi na kiusalama. Pia wanatakiwa kutoa mashirikiano na kuruhusu wahusika kuendelea na operesheni zilizopangwa bila ya kuwa na hofu yeyote. Pia wanatakiwa kuhakikisha wahusika wote wa mpango huu hawasibiwi na tatizo au kikwazo chochote.

Operesheni mahsusi zinazolengwa na mpango huu hazijafahamika mara moja hata hivyo kwa mujibu wa chanzo cha taarifa hii inaamika sana kuwa lengo ni kufanywa kwa mashambulizi ya risasi dhidi ya watu hususan watalii, maofisa wa kibalozi na viongozi wa dini. Pia kuripuliwa majengo mbali mbali hususan ofisi za kibalozi na majengo ya ibada.

Hivi karibuni Jeshi la polisi lilivamia Ofisi za Makao Makuu ya Chama cha Wananchi – CUF, Mtendeni Zanzibar na kudai kwamba ndani ya mejengo ya ofisi hizo kumeingizwa silaha na miripuko. Jambo lililoushangaza umma ni vile Polisi hao kufanya upekuzi huo wa kushtukiza katika ofisi zote, vyoo na dari bila ya kugundua silaha yeyote.

Viongozi wa CUF akiwemo Katibu Mkuu wa Chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad baada ya tukio la uvamizi wa Ofisi wa CUF Mtendeni alisikika akisema kwamba wanazo taarifa za uhakika kwamba sula la uvamizi wa Makao Makuu yao linatokana na jaribio lililofeli la kupachikiza silaha silaha ndani Ofisi hizo. Maalim Seif aliendelea kuhusisha tukio hilo na juhudi za Dola za kupigania kumakisha Dr Shein madarakani jambo ambalo kwa mujibu wa Maalim Seif ni jambo lishaloshindikana.

Share: