Habari

Ujenzi wa bandari Mkokotoni kutumia 1.5bn/-

May 13, 2018

NA HAFSA GOLO

SHIRIKA la Bandari Zanzibar linatarajia kutumia wastani wa shilingi bilioni 1.5 kwa ajili ya ujenzi wa gati na uzio katika bandari ya Mkokotoni iliyopo mkoa wa Kaskazini Unguja.

Mkurugenzi wa shirika hilo Kaptein Abdalla Juma alieleza hayo alipokua akizungumza na mwandishi wa habari hizi ofisini kwake Malindi mjini hapa.

Alisema ujenzi huo unatarajia kuanza wakati wowote baada ya kukamilika utaratibu wa kumpata mkandarasi.

Alitaja miongoni mwa mambo ambayo tayari yameshatekelezwa kwa ajili ya maandalizi ya ujenzi huo ni pamoja na kufanyika kwa zoezi la upimaji wa ardhi.

Alisema uchunguzi huo unafanywa na Kampuni ya Drilling and Dam Construction Agency kutoka Dar es Salam na unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi wa huu.

Mkuu wa Mipango na Utafiti wa Shirika la Bandari Zanzibar Ali Haji Haji, alisema jambo la msingi na linaloombwa na shirika hilo ni mashirikiano ya wananchi pamoja na serikali ya mkoa ili kukamilisha zoezi hilo kwa wakati.

Sambamba na hilo alisema katika kuhakikisha shirika linatoa huduma bora limeshanunua vifaa mbali mbali ikiwa ni pamoja na magari ya kubebea makontena.

Zanzibarleo

Share: