Ujumbe maalum

Mfuko wa MZALENDO.NET Foundation – Michango

Salaam,

Kwa bahati mbaya au nzuri hapa tuna mfuko wetu ambao ungetarajiwa katika nyakati ngumu kama hizi ambapo wenzetu wako ndani wakiteseka tungeliweza kuwasaidia.Kuwalipa haiwezekani, lakini kujitutumua angalau kuwalipia wakili pia tumeshindwa.

Tutapeana updates kuwa mfuko una dolla 2 mbili 200$, tunachukua nafasi kushukuru wazalendo wote waliochangia.Allah azidi kuwapa imani, na inshallah michango yao hio itatumika kwa lengo na nia iliokusudiwa.Fedha hizi ni kidogo mno, maana kusema hata unamlipia mmoja kati ya vijana wale dhamana basi hazitoshelezi.

Inshallah wazalendo wanaombwa wajitolee kwa wingi.Shukurani za dhati kwa waliochangia miezi mitatu ilipota:

1.Mohamed Saleh
2.Tawhiyd Muslims Org.

Wasalam

PS: Kuna tatizo la kiufundi ambalo tunalishughulikia kuhusiana na maoni, kwani inaonekanika wale wanaotoa maoni yao hayajitokezi. [stonetown]

Share: