Ujumbe maalum

Nidhamu utoaji maoni

Salaam,

Tumegundua kuna wazalendo wengi wameanza kujisahau na kutumia lugha chafu na zenye matusi katika utoaji maoni.Tunaomba wazalendo washirikiane na uongozi kwa kuwarepoti watoaji maoni hao ili hatua za nidhamu zichuliwe.

Tutalitazama tena hili la kuripoti, nadhani halijarahishwa kiasi fulani.Tumegundua wazalendo huona maoni yenye lugha chafu na kuamua kutochukua hatua, ikimaanisha pengine mtandao haujaweka miundo mbinu ya kuripoti makosa hayo.

Kwa mara nyengine tena tunawashukuruni kwa kueka nidhamu, lugha chafu ni suala ambalo halikubaliki ndani ya mtandao.

Share: