Ujumbe maalum

Shukrani za dhati kwa wazalendo

Salaam,

Imekuwa muda kidogo na harakati nyingi kutokea kiasi cha kuruka mambo mengi makuu na ya msingi likiwamo na lile la kutoa shukrani za dhati kwa wazalendo na wale wote wanaunga mkono mtandao.

Tunapenda kutoa shukrani za dhati kwa wale wote waliochangia mambo yafuatayo:

Michango ya Bi.Mwanaidi:

Harambee hii ilipita na wazalendo wengi kujitokeza na kuchangia, michango hio ilifikishwa kwa muda na mgonjwa huyo kufikishwa kwenye matibabu kwa muda Alhmdulillah tunashukuru kwa hilo.

Hosting ya mtandao:

Hivi karibuni kwa kutumia mfuko wa mtandao tumefanya malipo ya mwaka mzima ufuatao hadi 2015/12.Tumefanikisha hilo tunatoa shukrani za dhati juu hilo.

Iddi-Fitri:
Tunawakieni Iddi njema popote mlipo, Iddi Mubarak.

Wasalaam,

MZALENDO.NET

Share: