Ujumbe maalum

Tangazo: Uchapishaji wa habari ndani ya MZALENDO.NET

Salaam,

Uongozi wa MZALENDO.NET umekuwa ukipokea malalamiko mengi KIPINDI hiki kwa wadau na wazalendo wengine wanaotembelea mtandao huu kuwa habari nyingi ziandikwazo aidha zinakosa uaminifu au vyanzo vyake si vya uhakika.Utaratibu uliopo tukumbushana hapa habari zitokazo magazeti lazima mwisho kuandikwe chanzo, habari zisizo na chanzo mwisho ni zile ambazo mtu ameandika kwa maneno yake mwenyewe.

Tunaomba wale waliopewa haki za uchapishaji habari wawe makini na kuchapisha habari ambayo si ya uhakika.Kama habari si ya uhakika kwa maana haijatangazwa na mhusika tunaomba isichapishwe na kama itafanyika hivyo kuwe na tahadhari kubwa kuwa habari hio si ya kuaminika hadi wakati inapochapishwa au kutolewa.

Ndani ya MZALENDO.NET tuna category/gawanyo zima “Zenjilikis” ambalo ni mtindo wa habari ambazo hazijapata uhakika wakati zinapochapishwa.Tunarudia lazima habari ya namna hii iwe wazi kama si ya kuaminika.

Mwisho:
Kuchapisha habari yenye kichwa “BREAKING NEWS” wakati habari haina uhakika si suala la kuvumilika na hatua za nidhamu zitafuata kutoka kwa mafundi mitambo ikigundulika mchapishaji anafanya hivyo.Tutachukulia ni ubadhirifu wa nyanzo/resources ndani ya mtandao huu.

Tunatoa shukran za dhati kwa wadau wote waliochukua hatua za kutuhabarisha juu ya umakini wa habari na wazalendo wote – tuko pamoja kwa ushirikiano.

UONGOZI WA MZALENDO.NET

Share: