Ujumbe maalum

Ujumbe Maalum – kufuatia matatizo ya kiufundi

Salaam,

Kwanza naomba tujuzane kwamba ni kweli kumekuwa na tatizo kwa mda kidogo.Tatizo hizo kwa ufupi ni uhaba wa sehemu ya kuhifadhia data yaani hard-drive au disk ya computer yetu ambayo ina ukubwa wa 20G.

Baada ya mchakato wa hapa na pale nimeweza kujaribu kutafuta njia muafaka ya kutupa muda wa kuvuta pumzi, leo afadhali kidogo nimeweza kusave 18% ya kuwa free kwa ajili ya matumizi ya mtandao na vile vile kueka mchakato ndani ya DB ili kuweze kufanyika ‘rotation’.Sehemu kama ya 5G ilikuwa imebanwa na DB files ambazo zinaweza kuwa rotated.

Hali ilivyo sasa:

Filesystem Size Used Avail Use% Mounted on
/vz/private/2384 20G 15G 5.7G 72% /

Nashauri kama uwezo upo basi kuongezwe disk space ntalifanyia utafiti kidogo hili kujua litagharibu vipi.

Vyovyote iwavyo kwa muda wa sasa mambo shwari.

Wasalaam,

Share: