Ujumbe maalum

Ujumbe maalum – Kadhia ya viongozi wa kiislamu kudhalilishwa

Kwenye maada za Masheikh na viongozi wetu wa kiislamu kila ataeonekana anatoa maoni kinyume na matarajio ya waislamu na wazanzibari tunamchukulia hatua za nidhamu mara moja.

Tukubaliane moja kuwa viongozi wote walioko nyuma ya mtandao huu ni waislamu na wanatokea Zanzibar.Hii tunakusudua kuonesha kama tuko upande wa kuwatetea viongozi masheikh hao.

Alie na maoni tofauti na hayo akae pembeni au akatolee maoni hayo kwengine.Kwa muda huu ambao wengi wetu nyoyo zinatuuma kila tukifungua habari ni Sheikh kadhalilishwa hatukubaliani na kuwa mtandao huu uendelee kutumika kama njia ya muendelezo wa dharau dhidi ya viongozi wetu wa kiislamu.

Masikhara au aina yoyote ya dhihaka hairuhusiwi kwenye maada yoyote inayowahusisha Masheikh na viongozi wa dini.

Wasalaam
UONGOZI WA MZALENDO.NET

Share: