Habari

Umasikini wa Pemba maoni yangu sehemu ya 1

Kufuatia mjadala uliojitokeza kuhusu hali ya umasikini unaoikabili Pemba pamoja na michango na maoni ya wananchi wengine juu ya hali hii, nami leo nachukuwa nafasi hii kuangaza na kutoa baadhi ya yale ambayo nimegundua huko Pemba.

Nimepata fahamu zangu katika miaka ya katikati ya 80s, nikiwa bado mengi nayakumbukia. Moja ya misemo au dhana kubwa tulokuwa nayo wakati huo nikuwa wasomi wengi wanatoka Pemba. Baada ya mabadiliko ya kiouongozi na kisera yaSerikali ya mapinduzi ya Zanzibar, wananchi wa Pemba walikuwa mstari wa mbele kuchangamkia fursa zilizojitokeza. Hivyo kukajengeka dhana kuwa wafanya biashara wengi na wakubwa ni Wapemba.

Kushamiri kwa vuguvugu la kupigania demokrasia nchi Zanzibar nalo lilibeba dhana nyengine ya tatu, kuwa Pemba ni sehemu iliyoimarisha kupinga dhulma na kupigania demokrasia. Hadi kufikia mwanzoni mwa 90s dhana tatu hizi ndio zilikuwa zimenawiri ndani ya fikra za watu wengi, kuwa; wapemba wamesoma, wafanya biashara wakubwa, na mstari wa mbele kupigania demokrasia.

Bado sina takwimu halisi hadi sasa kuthibitisha dhana hizi kama vile wakati ule ni wapemba wangapi walikuwa wamemaliza degree, Master au PhD. Halkadhalika ni kiasi gani wafanya biashara wa Pemba walikuwa wakimiliki au share market yao ilikuwa asilimia ngapi. Ama kwa upande wa kupigania demokrasia hili vielelezo viko wazi. Kwamba walisimama kidete na kuwa ngome imara ya chama cha upinzani hadi leo hii. Pia tukikumbukia roho za watu zilizopotea na damu iliyomwagika kupigania demokrasia ni asilimia kubwa ukilinganisha na idadi ya wakazi wake.

Utafiti unahitajika kujuwa ni kiasi gani cha Wapemba wamesoma. Pamoja na hili la wafanya biashara na mitaji yao.

Huu ni wakati muafaka wa kufungua mjadala wa wazi kujuwa chanzo cha umasikini wa Pemba, sababu zake na mwisho tutaweza kutatua na kuondosha umasikini ndani ya Pemba. Mjadala huu usiwe wa kutukanana wala kudharauliana, Uwe ni mjadala wa heshma na kusikilizwa kila mmoja na mawazo yake. Lengo nikuona INAWIRI PEMBA na ustawi wa watu wake.

Juhudi za kuanza kufanyia kazi hayo yote tayari zimeanza. Najuwa zipo taasisi tayari zimeanza nami nikiwa mmoja wapo. Ingawa hili sio la mmoja ndio nikakaribisha michango na maoni mbalimbali yatakayoweza kusaidia kwenda mbele.

Share: