Habari

UMASIKINI WA PEMBA MAONI YANGU SEHEMU YA 3

UMASIKINI WA PEMBA MAONI YANGU SEHEMU YA 3
 

 01/12/2017 

Nikiendelea na uchambuzi juu ya umasikini wa Pemba leo nitaangalia zaidi infrastructure (miundombinu).

Pemba imegawika katika Wilaya 4 ambazo kila wilaya imebahatika kuwa na Hospital yake. Kwa jumla Pemba ziko hospital 4 kubwa ambazo ni Abdalla Mzee Hospital, Chakechake Hospital, Wete Hospital na Micheweni Hospital. Wananchi wengi wa Pemba wanayo fursa ya kuchaguawa moja kati ya hospital hizi kupata matibabu. Abdallah Mzee ndio inayoongoza kwa hadhi licha ya kuwa na vifaa duni kulingana na maendeleo ya technology na health advancement. Mfano Abdalla Mzee inayo ECG machine ukubwa wake ni size ya 10 inch tablet (tab), wakati hizo electrodes zake pamoja na kunyolewa nywele za kufua hazigandi. Huku Wete Hospital ikiwa ya mwisho kwa majengo machakavu, madokta, wauguzi, matibabu, dawa na huduma. Pemba hakuna hospital ya private bali ziko private dispensary.

Kwa upande wa skuli Pemba ina jumla ya skuli 9 za private, hii ni kwa mujibu wa takwimu ya Wizara ya Elimu. Utafiti unaonyesha kuwa kuna skuli 5 za private ambazo ni Iqraa (wete), Istiqama (Kinyasini), Laureate (Ole), Samail, na Mabaoni. Hizi ni skuli za secondary. Ambazo zimekusanya na primary pia.

Miaka ya karibuni vyuo vikuu vya Zanzibar vimefungua branch huko Pemba ikiwa ni Pamoja na State University of Zanzibar (SUZA), Zanzibar University, Institute of Public Admin (IPA). Kipo Chuo cha Ualimu, Mchangamdogo. Kwa upande wa vyuo vya Private Pemba iko nyuma sana. Chuo maarufu na cha mwanzo kilikuwa Dar Institute ambacho kilikuwa na matatizo kadhaa wa kadhaa hadi kufikia kufungiwa.

Pemba kuna library moja ambayo ipo Chakechake. Kuna taarifa nyengine zinasema pemba kuna Library tatu; Moja ipo Wete na nyengine ipo Wingwi. Library ya Chakechake ina vitabu chini ya 1000 ambavyo ni vya zamani sana. Vingi vikiwa ni vitabu vya fiction.

Kwa upande wa barabara Pemba inayo transPemba high road kuanzia Mkoani hadi Konde, ambayo imegawika kupitia Wete na nyengine kupitia Wingwi. Licha ya Pemba katika miaka ya karibuni imeweza kujengwa barabara nyingi lakini ziko chini ya kiwango na zimeanza kuharibika. Ambapo jicho la huruma linaiangaza barabara ya Chake-Wete licha ahadi kadhaa na kuwa katika hali mbaya sana. Ukiachia barabara hii, nyengine zilizobakia zina afadhali. Ziko barabara nyengine ambazo zimeongezwa hadhi kuwa za kifusi. Barabara ya Mapofu-Chimba, Tumbe-Finya, Ole-Kengeja, inaelekea kuwa ya kiwango cha lami, etc.

Pemba imebahatika kuwa na bandari mbili zinazounganisha sehemu mbili muhimu. Bandari ya Mkoani imekuwa link muhimu baina ya ya Pemba na Unguja, wakati bandari ya Wete imekuwa kiunganishi baina ya Pemba na Tanga. Hivi karibuni kumezinduliwa bandari nyengine ya Micheweni. Hii ni fursa nyengine muhimu kwa Pemba kwa vile itaweza kuwa link baina ya Pemba na Mombasa.

Usafiri wa anga Pemba inao uwanja mmoja ambao hauna uwezo wa kutuwa ndege kubwa. Hata hivyo umeweza kwa kiasi kikubwa kusaidia usafiri wa haraka na dharura kutoka na kuingia Pemba. Bado hakujawa na mipango ya uhakika kuufanyia matemngezo uwanja huu.

Mnamo mwaka 2010 Pemba imefanikiwa kuapata umeme wa uhakika. Umeme kutoka tanga hadi Pemba ulizinduliwa mwaka huo na kuwaondoshea wananchi adha waliyokuwa nayo kwa miaka kadhaa. Kumekuwa na ongezeko kubwa la wananchi kuunga umeme kwa matumizi yao na biashara. Ingawa Shirika la Umeme (ZECO) linaudhaifu wake kama vile kuzimika, kupanda na kushuka (fluctuation), kutojali wateja (nimeona nguzo imeanguka, kufika jioni mafundi wanasema “itakuwa nini kukosa umeme siku moja”). Sasa hivi kuna majaribio ya kuzalisha umeme kwa upepo ambapo vituo viwili vimefunguliwa Micheweni na Muambe.

Pemba ina barka ya maji ingawa utaratibu mbovu na udhaifu wa mafundi wetu unapelekea wananchi kukosa maji safi. Wananchi wanalipia maji bila kupata huduma hii, kila wilaya inakuwa na usimamizi katika eneo lake. Nimekwenda kuonana na Mkuu wa maji Pemba kupeleka malalamiko yangu, naye alinipeleka kwa Afisa Maji wilaya ya Wete.

Mawasiliano ya simu kumekuwa na ubora kuliko siku za nyuma, licha ya kuwa coverage na reception ni mbovu. Data maeneo kadhaa inapatikana ingawa speed yake ni mbovu au huwezi kupata voice call. Kuna radio tatu ndani ya Pemba, ambazo ni Radio Jamii Micheweni, Radio Istaqama Chakechake, na Jamii Mkoani. Pemba inategemea matangazo ya TV kutoka vituo vyengine kwani hakuna kituo cha TV ndani ya Pemba.

Pemba imebahatika kuwa na uwanja cha Mpira wa miguu, Gombani Stadium, ambao unaendana na mazingira. Mkabala na uwanja wa mpira kumejengwa uwanja wa mchezo wa judo ambao unaanza kushamiri kwa kasi. Pia kipo kiwanja kimoja cha kufurahishia watoto, Tibirinzi.

Share: