Habari

upinzani watoa tamko zito kuhusu hali ya domokrasia Tanzania

‘Azimio la Zanzibar’ limetiwa saini na viongozi wa vyama sita vya upinzani vilivyokutana kuanzia jana Jumatatu (Disemba 17, 2018) Verde Hoteli, Mtoni-Marine, Zanzibar. Majina ya viongozi na saini zao kama yanavyoonekana kwenye picha. Picha kutoka mpekuzi blog

Kutoka Verde Hoteli, Zanzibar
Jumanne, Disemba 18, 2018

Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe amesema vyama sita vya upinzani nchini Tanzania vilivyotoa tamko la pamoja leo Jumanne, Desemba 18, 2018 vimeazimia kuutumia mwaka 2019 kudai demokrasia.

Akizungumza na Gazeti la Mwananchi baada ya Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad kumaliza kusoma tamko hilo, Zitto amesema Tanzania kuna ukiukwaji wa demokrasia, na kubainisha kuwa bila kupambana, hali ya vyama vya upinzani itakuwa ngumu zaidi.

Amesema kila mmoja anapaswa kupambana na hali ya mgogoro wa kidemokrasia, lazima wajitoe kupigania jambo hilo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia amesema waliyokubaliana Zanzibar, yatatekelezwa kwa vitendo kwa sababu ni maelekezo yaliyopo hata katika katiba ya nchi.

Amesema kutokana na ukiukwaji wa demokrasia ni lazima kila mtu apambane kudai haki vinginevyo mambo makubwa zaidi yanaweza kutokea.

Leo (Jumanne, Disemba 18) vyama hivyo sita vilivyofanya mkutano wa faragha wa siku mbili mjini Zanzibar, wametoka maamuzi mawili mazito.

Katika mkutano huo uliyoandaliwa na CUF kupitia Maalim Seif,  wameazimia kuanza kufanya mikutano ya hadhara kwa kuwa ni haki yao kwa mujibu wa sheria na katiba ya nchi.

Pia, wametangaza rasmi kwamba wanasiasa wote waliopo magerezani kwa tuhuma za kisiasa watatambuliwa kuwa ni ‘wafungwa wa kisiasa’. Na kuanzia sasa wataitangazia dunia hivyo.

Tamko hilo limesainiwa na Maalim Seif, Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia, Mwenyekiti wa NLD, Oscar Makaidi, Naibu Katibu Mkuu wa Chadema-Zanzibar, Salum Mwalimu, Mwenyekiti wa Chaumma, Hashim Rungwe na Kiongozi wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe.

Vyama hivyo vimetoa uamuzi huo wakati Serikali ya Tanzania ikiwa imepiga marufuku mikutano yote ya kisiasa ya hadhara mpaka mwaka 2020.

Miongoni mwa viongozi wa upinzani waliyomahabusu ni pamoja na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na mweka hazina wa Baraza la Wanawake la Chadema (Bawacha), Esther Matiko ambaye pia ni mbunge wa Tarime Mjini.

Awali, Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad akizungumza na waandishi wa habari baada ya kikao cha siku mbili cha vyama sita vya upinzani, alisema mwaka 2019 ni mwaka ambao watapambana kwa hali zote katika kudai haki zao wanazonyimwa kinyume na katiba na sheria za Jamuhuri za Muungano wa Tanzania.

“Kama vyama vya siasa vyenye uhalali na utaratibu uliyowekwa rasmin kikatiba, tunatangaza rasimi namna ya kufanya mikutano yetu ya hadhara katika kila kona ya nchi yetu,’’ alisema Maalim Seif.

Alisema hawatoruhusu katazo haramu ambalo alisema linakwenda kinyume na sheria za nchi na kudai haliwezi kuzuia kazi zao. Maalim Seif ni mwanasiasa aliebobea katika siasa za Tanzania na nje.

Aliwataka wanachi pamoja wanachama wote wa vyama sita, wakati ni sasa wa kuondoa hofu na kuunga mkono vyama vyao ili kulinda demokrasia.

“Hatupaswi kuwa woga hata kidogo na hatupaswi kujisalimisha katika kudai haki zetu kama mtu mmoja au kikundi, lazima tupeleke ujumbe huu wa uhuru na demokrasia kwa viongozi wenzetu wote’’ alisema Maalim Seif.

Sambamba na hilo alitangaza kuanzia siasa, Freeman Mbowe na Esther Matiko (CHADEMA) ambao hadi sasa wako mahabusu kuwa ni wafungwa rasmi wa kisiasa na kueleza kuwa tangazo hilo halitofutwa mpaka pale watakapoachiwa.

“Tutapambana kwa nguvu zote kuhakikisha wafungwa wote wa kisiasa, nchi nzima wanapewa nafasi ya kupata haki katika mfumo uliyohuru mbele ya mahakama na macho ya watu,’’ alisema Maalim Seif ambaye aliwahi kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar katika Serikali ya Umaoja wa Kitaifa.

Kupitia mkutano huo, Mwenyekiti wa Chama cha UMMA, Hashim Rungwe alisema hawawezi kumruhusu mkandamizaji wa siasa aendelea kuwakandamiza wanachi na demokrasi na kueleza, sasa basi.

“Lazima tuwaeleze wananchi wakatae utawala huu wa kibabe kwani ndio uliopomorosha maisha yao’’ alisema Rungwe.

Alisema kuwa demokrasia ina gharama na wakati ukifika watawaeleza nini watafanya katika kupiga vitendo vya uvunjwaji wa demokrasia.

Akizungumza katika mkutano huo ambao ulitoka na tamko la ‘Azimio la Zanzibar’ Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia alisema hali iliyopo sasa ni kutokana na ubinafsi wa utawala uliopo.

Alisema kuwa ubinafsi huo ndio uliopelekea maisha ya watu kubadilika na kuwaona wengine ndiyowalio na haki hapa nchini.

Kwa pamoja wakizungumzia kuhusu suala la Zanzibar, vyama hivyo vilitoa tamko na msisitizo kuwa hawaitambui serikali ya inayoongozwa Dk Ali Mohamed Shein na kusistiza kuwa ni serikali haramu kutokana kile walichodai kupora ushindi wa CUF mwaka 2015.

Akizungumzia kuhusu baadhi ya wabunge na madiwani waliyohama kutoka upinzani na kujiunga CCM, Waziri Mkuu wa zamani, Frederick Sumaye alisema viongozi hao hawakuhama bure na wameenda huko kufanya biashara ya kisiasa.

“Unapoona wabunge na viongozi wa upinzani wanahamia chama tawala ujue chama tawala kimefika mwisho kutawala katika nchi…Hapa ni dhahiri CCM wamefika mwisho wa kutawala Tanzania,’’ alisema Sumaye.

Chanzo: kutoka katika mitandao ya kijamii..

Share: