Habari

Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania/Kauli la Waziri M.Aboud.

Tunakubaliana kimsingi kuwa Tanzania ni :
Muungano wa nchi/Taifa/Dola mbili huru zilizokubaliana kuungana pamoja kwa mambo Maalum
baina Viongozi wa Dola Mbili Huru .
Kwa upande wa Zanzibar akiwa Marehemu A.A.Karume na kwa Upande waTanganyika akiwa
Marehemu J.K.Nyerere.
Marais hao wawili walikubaliana kufanya hivyo kwa niaba ya Wananchi wao,lakini bila ya Kuwauliza
au kuwataka fikira wananchi wa nchi zao mbili husika .
Walifanya hivyo kwa wadhifa na nguvu zao wakiwa ni viongozi na Maraisi wa nchi zao mbili na
hapakuwa na sheria au kipingamizi chechote cha kikatiba ambachokingeweza kuwazuwiya
kufanya hivyo,kwa wakati Ulee.
Mikataba au makubaliano kama hayo yamefanyika sehemu nyingi duniani,baina ya viongozi wa kisiasa
au hata wafalme katika nchi mbali mbali – mfano USA,UK,UAE na Ujerumani auiliyokuwa ikiitwa
Union of South Africa etc.
Miongoni mwa makubaliano hayo ni kwamba,ataendelea kuwa Rais waZanzibar,serikali yake na baraza
lake la Mapinduzi .
Rais wa Zanzibar wakati wote na daimaanachaguliwa na wananchi wa Unguja na Pemba- Zanzibar.
Hapana Mtanganyika anaemchaguwa Rais wa Zanzibar – hiyo ni wazi kabisa .
Rais wa Jamhuri ya Tanzania anachaguliwa moja kwa moja na wananchi wa pande zote mbiliyaani
Zanzibar na Tanganyika na mtetezi wa wadhifa huo alikuwa anateuliwa na chama CCM chama tawala,
lakini hivi sasa wadhifa huo wa Urais unaweza kugombaniwa na Mtanzania yeyote kutoka
Chama Chechote ikiwa ni wa kutoka Pemba,Unguja,Tabora,Dodoma,Shinyanga,Kigoma au Mafia
na sehemu nyingine zote za Tanzania .
Kwa hivyo,ile habari ya kua eti “watu wanafikiri ndani ya boksi moja tu la CCM” halipotena
limekwenda arijojo,hali nguvu tena uamuzi upo kwa wananchi wote kutoka vuama tofauti.
La kuuliza hapa ni jee katika huu mkururo wa vyama vya kitaifa vyenye wanachama kutoka Bara  na
Visiwani inawezekana au haiwezekani kuwepo  Mtetezi wa Kugombeya Wadhifa wa Urais kutokaWawi,Wesha,Mbweni, Kwa Mtipura,Uzini au  Kigurunyembe au kutoka kijiji kiitwacho Matombo ?
Jee tuseme endapo Rais wa Tanzania hata chaguliwa moja kwa moja na wananchi kwa mujibuwa
(universal Sufferage) bali atakuwa anachaguliwa na Bunge, kwa mujibu wa baadhi ya fikra za baadhi wananchi,hapatokuwepo dhulma ya kuwanyima wananchi wengi uhuru wao wa kumchaguwa mtuwamtakaye kushika wadhifa huo wa Uraisi ? 
Ikiwa ni Bunge ndilo kitakalo fanya hivyo,basi Bunge litakuwa na nguvu zote za pekee za kuwezakulazimisha
na kuwasakamiza wananchi wawe chini ya Rais bila ya radhi na idhini ya Umma.
Rais huyo atakuwa ni wa/kwa wananchi au atakuwa ni wa Bunge linalotawala nchi ?
Na hiyo serikali itakuwa ni ya Ushirika/Mseto wa vyama vyote viliomo Bungeni ?
Ikiwa uchaguzi wa Rais ufanyike Bungeni,kwa hivyo lazima jambo hilo lifanyike kwa kufuatiya njia za katiba
ya Muungano – na katiba hiyo itabidi ikubalike kwa mujibu wa maoni na kura zaWatanzania – jee jambo hilo litaweza kupatikana kwa idhini ya watu wa Bara na Visiwani  ?
Jee Zanzibar katika majadiliano ya katiba ya Tanzania ,itowe kua  Sharti lake muhimu la kuwemo
kwake kwenye Muungano, basi  Urais wa Tanzania uwe kwa Zamu baina ya Mzanzibari na Mtanganyika?
Na ikiwa si hivyo inajitowa kwenye Muungano? 
Tamko la kutaka kuwepo Urais wa Tanzania kwa Zamu/Kuzunguka baina ya Bara na Visiwani.
Tamko au fikira hiyo ilikuwa ikizungumzwa sana ,na hata hivi karibuni Seif Shariff,aliiletat ena hadharani,
lakini hakuja na Hoja Yeyote Kamilifu Ya Kimsingi, ilaa tu/isipokuwa ni zile hisiya-khamasa za
kuvutiya umma kusikia wapendacho kusikia (Populistic -insular mentality) za Uvisiwani zenye lengo
maaalum la kisiasa ambalo halisimikwi/si sambamba na ule utiliaji nguvu wa muunganisho wa utaifa la
Utanzania, bali ni kutaka kusambaza ” Usisi ” na “Uwao “,yaani “Sisi Wazanzibari” na
Wao Watanganyika ” wakati ambapo panatakiwa kujadidisha Utanzania .
Utanzania kwa sababu  Rais wa Tanzania ni Rais wa pande zotembili  za  Muungano,ingawaje Wazanzibari wanae Rais wao mwenye wadhifa kamilikwa mambo yote
yasiyo ya Muungano kikatiba.
Ukosefu au tofauti ya muelewano wa kiini,sababu,itikadi na shabaha za Muungano ndipo panapoleta utata .
Utata na tofauti za kiitikadi baina ya wananchi,na baina wanasiasa wa vyama tofauti.
Na utata huu si, maajabu bali ni umbile la Ubinaadam, sisi sote si sare kifikira wala kimalengo ya mipangilio
ya kimaendeleo.Ni watu wamoja,lakini wakitafauti 
Utata wa mwingine,ni ule unaotokana na ama Kuutaka au Kutoukataa  Muungano.
Kauli ya Waziri M.Aboud,akiwa ni mwanachama wa chama tawala au kama nimwananchi wa
kawaida kama wengine wote ana haki hiyo ya kujitamka huru jinsi yeye aonavyo kama vile Seif Shariff ,Amur,Mohammed,Fisal,Pandu,Jecha au Achumani.
Mfano uliotolewa na ndugu Rifkha wa nchi ya Uswisi kuhusu Urais wa zamu hauwezi kuhalalisha yahuko yakubalike katika nchi kama Tanzania kwa sababu ya mazingara halisi ya mchanganyiko wa kijamii na mfumo
wa kitawala uliopo katika nchi mbili zilizotofauti sana kwa mengi, kihistoria na utamaduni.
Hali kadhalika ni kama vile alipokoseya kuja na ule mfano mwingine kuhusu mfumo tawala wa Libanon.
Mifano yake hiyo miwili yaani Uswisi na Libanon basi tafauti zake ni kama mbingu na ardhina kufananisha hizo
na Tanzania ni kama North na South Pole Kimawazo, Utamaduni na hasapirika pirika za Kihistoria na taratibu
za kitawala.
Isitoshe wale wanaopendelea mambo ya kuigiza igiza ile mifumo tawala ya njee kuwa ni bora kufuatwa Tanzania ,basi tunaweza kujikuta katika majanga ya kipotoshi na wengine tunaweza kusema na kuulizabasi
kwa nini hatufuati mifumo kama ya Uingereza,Indonesia,Urussi au Marekani .
Kwa mfano, George W.Bush,alikuwa rais na Baba yake nae alikuwa Rais – kwao kule hapajakuwa na utata
wa kimsingi wa aina yeyote ile ;chama kilipendekeza Bush akapita na akachaguliwa.
Lakini jee kesho endapo Ali A.A.Karume,atawania wadhifa wa Urais wa Zanzibar au wa Tanzania –Mtasemajee ???  Suala la “Haki Sawa ,Kwa Wote ” litazungumzwa vipi,kiverejee?
Kwa hivyo ,ile haki ya Kugombania Urais wa Tanzania isiwe kwa zamu baina ya nchi mbili zilizomo
katika Muungano,bali iwe ni haki kwa kila Mtanzania ,yeyote mwenye sifa zoote zinazokubalika kikatiba
bila ya kujali asili,chama au sehemu atokayo katika eneo lote la Muungano wa ardhi ya Tanzania.
Share: