Habari

Ushauri wa kiusalama dhidi ya mazombi

Kwa muda tumekuwa tukisia vitimbi na vitisho.Kiukweli na tunataka iaminike kuwa vikundi vinavyoleta fujo vina imani ya kuwa havitopata majibu na wazanzibari watakaa wakilia-lia pembezoni.Hivi vikundi kama mazombi vinabadilika majina tuu.Miaka ya zamani vikiwa na majina kama janjaweed na sasa vikibandikwa majina ya mazombi.Nadhani ni hao hao tuu, na hatubahatishi hivi ni vikundi vya SMZ kama JKU n.k. ambavyo vina ushirikiano na vile vya ulinzi vya Tanganyika.

Kinachosikitisha hapa ni kuona wananchi wakijiinamia kama vile hawana mikono au hawajui kutia makali mapanga.Hiki ndio nataka nitoe rai kwa zama hizi za leo ukizingatia mawasiliano ya mitandao na masimu yaliojaa.Nitarudia hapo mbele jinsi ya matumizi ya mitandao na jinsi gani yanaweza kutumika kujipanga na kujihami dhidi ya uovu katika mitaa, vijiji na vitongoji tunavyoishi na familia zetu.Ni lazima tuhakikishe na kwa uwezo tuliopewa na Allah kujihami na kulinda familia zetu.Hili ni jukumu letu si la mwengine.

Ushauri wangu sio mpya miaka ya zamani imetumika sana kueka askari wa kijamii kila kitongoji kulinda wezi na majambazi.Nadhani muda sasa umeshafika wazanzibari wa kila kitongoji wakaunda vikundi vya kujihami na wote wakawa na mtandao ambao kila ataevamiwa usiku anawasiliana kwa kutoa taarifa ya dharura kwa askari jamii ambao wanazuka haraka kwenye tukio na kurekebisha mambo au kutoa suluhusho.

Nadhani hii ni njia rahisi na hahitaji leseni wala unifomu.Isifike hadi sehemu tena tunavamiwa majumbani na mazombi na wananchi wakawa wamekaa tuu na kujinamia chini.Hii inasikitisha kiufupi waliotarajiwa kulinda sheria na watu wake, wao ndio wako mstari wa mbele kuzivunja.Hapo sitarajii kusikia waliosababisha kifo kufikishwa mahakamani wala kutajwa, watabakia ‘wasiojulikana hadi kiama’.

Wasalaam,
Allah alete subra katika kipindi hiki kigumu.

Share: