Habari

Utandawazi chanzo cha wanafunzi kutofanya vizuri skuli

March 6, 2018

Imeandikwa na Khadija Mahmoud , Pemba

Afisa Elimu Mkoa wa Kaskazin Pemba Mohd Nassor amesema suala la utandawazi linachangia kwa baadhi ya wanafunzi kutokua na maadili mazuri na kupelekea wanafunzi kukosa nidhamu Mashuleni.

Ameyasema hayo wakati wa Uzindunzi wa utekelezaji wa shughuli za nidhamu Utoro wa pamoja na Ukakamavu wa wanafunzi wa Mkoa wa Kaskazini Pemba iliyofanyika katika katika Skuli ya Mitiulaya Wete.

Amesema suala la Utandawazi limepelekea kwa wanafunzi kutokufanya vizuri katika mitihani yao pamoja na wengi wao kujihusisha na masuala ya kujiingiza katika vikundi viovu.

Nae Afisa nidhamu Utoro na Ukakamavu Mussa Saleh Said amesema amewataka wazazi kutoa ushirikiano wao ili kuhakikisha wanafunzi wanafuata nyenendo zilizo bora na kufanya vizuri katika mitihani yao.

Hata hivyo wanafunzi hao wameahidi kutekeleza na kufuata ushauri uliotolewa juu ya kuacha matendo maovu yanayosababisha kutofanya vizuri katika mitihani yao.

Pembatoday

Share: