Habari

Uteuzi wa Manaibu Mabalozi, Hakuna Mzanzibari….!

Jana Rais wetu mstahik Jakaya Mrisho Kikwete, amefanya uteuzi wa Manaibu Mabalozi kuwakilisha TZ nchi za Nje; bahati mbaya au nzuri — hakuna Mzanzibari hata yule ‘kuchovya’.

Hivi tuseme hakuna Mzanzibari, aliyetimia CCM 100% anayefaa kushika nafasi angalau ya Unaibu au Ukaimu au hata usaidizi na utarishi wa ofisi zetu za kibalozi. Unajua, ukwlei hasa ni kuwa Zanzibar inamahitajio yake tuseme ‘ya ziada’ au special kuliko yale ya Tanzania/Tanganyika (tuseme zaidi katika areas za kiuchumi, kiutamadauni), iwe iwavyo Zanzibar na Tanganyika ni nchi mbili tofauti, ndio kweli ‘zimeungana’ basi ndio Zanzibar ipigwe bao na Tanganyika kiasi hicho?

Niliandika siku za nyuma kuwa JK alifanya uteuzi wa mabalozi, na hakuna Mzanzibari hata mmoja, hata ile nafasi iliyowachwa wazi ya Balozi Mohammed Mwinyi Mzale (Sweden) haikupata mbadala wake. Suala hili lilizungumzwa Bungeni, na matokeo yake Mbunge wa Zanzibar alitukanwa matusi ya nguoni, na yule mbunge mwenzake Ally…wa Songea.

Tuseme hakuna msomi au mtu mwenye maarifa kutoka Zanzibar mwenye akili kama Mtanganyika, basi hao Wazanzibari wawili-watatu wlaiobaki katika ofisi za Kibalozi, si angalau JK awafanyie promotion then transfer kwenda huku na kule? Hii simple managerial thinking, unampandisha mtu cheo, then, anakuwa fulani bin fulan….

Hivi kweli Wazanzibari ndio tumekaa na kuzubaa tuuuuuuu huku tukidekeza matakwa ya CCM na serikali zao. Mimi sisemi ateuliwe CUF au Chedema, nitarkuwa radhi ateuliwe CCM 100%, tena mwenye kadi ya ASP — lakini awe Mzanzibari. Ninachikiona mimi kila siku zinapokwenda mbele, ‘Zanzibar is losing grip /ground kwa Tanganyika’ kwa areas zote

Ahsante sana Bwana Kikwete; na Karibu Zanzibar ufungue Ijtimai leo.

Share: