Habari

UTIAJI LAMI WAENDELEA BARABARA YA OLE-KENGEJA

December 6, 2017

KAZI ya utiaji wa lami kwenye barabara ya Ole- Kengeja yenye urefu wa kilomita 35, inaendelea vyema, ingawa hadi sasa ni kilomita 5 pekee, ambazo tayari zimeshawekwa lami, ambapo ni kuanzia Ole hadi hospitali Changuo Vitongoji wilaya ya Chakechake.

Barabara hiyo inajengwa na wizara husika ya Ujenzi ya SMZ, ambapo ikimalizika itawasaidia hata wananchi wanaotokea Wete kwende bandarini Mkoani moja kwa moja, kwa kupitia Ole, Vitongoji, Pujini, Chambani, Ukutini, Kichaka, Ndaambani, Vizuke, Kendwa, Muwani, Nanguji, Sipwese, Kengeja hadi Mtambile kuelekea Mkoani Bandarini.(IMEANDIKWA NA MWANDISHI WETU)

Pemba Today

Share: