Habari

Video:Kilio cha familia za waliotekwa Pemba

Nidokeze tuu kuwa kujihami au kulinda makaazi yetu sio kuvunja sheria wala katiba ya nchi.Kila mwananchi anayo haki ya kujihami na kuishi salama katika kijiji chake na nyumba yake na familia yake.

Nashauri wazanzibari wakajidhatiti kwa hili kwa kuunda vikosi vya kijamii vya kuratibu ulinzi.Silaha za jadi kama mishale, mikuki, mapanga n.k zipo na vijana katika vitongoji vyetu tunao.Kinachotakikana ni wazee kuwapanga vijana na kuanza doria inapoingia giza na hata ikiwezekana kweupe mchana kupiga doria kuhakikisha gari za ajabu ajabu haziingii.

Wananchi wakijipanga na kueka resistance itasaidia sana unyama huu unaofanywa na vikosi vya ulinzi kukoma au kusababisha watawala nao kufikiria mara dufu kabla hawajafanya mambo ya kishenzi ya namna hii.

Nakumbuka miaka ya zamani kulikuwa na mawazo / concept ya ‘sungu-sungu’. Hawa walikuwa ni askari wa kijiji wala hawatokani na serekali wakilinda mitaa yetu na kutoa ulinzi stahiki unaohitajika.

Nasikitishwa na kusononeshwa kuona wazanzibari na ndugu zangu wakikaa tuu bila ya kuchukua hatua za kujihami. Nafahamu kama hawa watu wana silaha za moto, lakini pia nafahamu kama wao ni wageni wa vijiji na makaazi yetu. Tutumie nyenzo tulizonazo kujihami, sijasema kuanza vita nazungumzia kujihami dhidi ya uovu.

Mtu alievamia kijiji na silaha na kuanza kuteka watu. Sitaki niamini kama anatokea vyombo vya ulinzi ni sawa na mwizi au mhalifu mwengine tuna kila sababu ya kuonesha kama tuna uwezo wa kulinda familia zetu pamoja na makaazi yake.

Nimalizie kwa kutoa pole kwa ndugu na familia zilizoathirika moja kwa moja na matukio haya.

Share: