Habari

Video:Tofauti za kimawazo – Mimba za wanafunzi

Nimeona nizungumze kidogo juu ya hii maada kuhusiana na wanafunzi wanaopata mimba.Tukubaliane kitu kimoja nimegundua tofauti kubwa ya kimtazamo juu ya hili suala.

Kwanza kabla sijaendelea na mjadala huu, kwa wale waliokuwa hawajaisikia kauli ya Mh.John Magufuli basi waendelee kuisikiliza hii kauli kwanza:

Wakati mabunge ya wenzetu yakijadili ni jinsi gani serekali itaweza kuwasaidia watoto waliopata uja uzito kuendelea kumaliza masomo yao.Tunajikuta waafrika tukijadili ni jinsi gani ya kuweza kuwasimamisha wasiendelee na masomo.

Nakumbuka mijadala ya aina ilikuwepo kipindi cha nyuma lilipokuja suala zima la seks education kwenye maskuli.Lazima ifike wakati kidogo uswahili tueke pembeni na tujaribu kuenda na takwimu.Wengi walikuja na mawazo kama haya kutoa elimu hii itahamasisha matendo ya ngono hadi watu walipoona vijana wakiteketea ndio tukaanza kueka jitihada zinazostahiki.

Najua kuna watakao niriukia na aya na mawaidha, lakini takwimu hazidanganyi na sote tunafahamu dada zetu, wenetu na ndugu zetu welivyokosa nafasi za kuendelea na elimu kwa kupata uja uzito wakiwa bado wako maskuli. Kiukweli nimesikitishwa na kauli ya Mh.Magufuli kwenye suala hili.Hili ni pigo tena kubwa katika jitihada za kuleta maendeleo na ukombozi dhidi ya umasikini.

Sitaki niamini kama mtoto aliejifungua na kumwacha mtoto kwa mama yake akaendelea na masomo atakuwa anawafundisha na wenzake jinsi ya kupata uja uzito.Hii ni kauli kidogo nadhani haitowi uzito unaostahili wa suala lenyewe {najaribu kuwa makini na lugha nisije pewa kesi ya uchochezi :D}

Wasalaam

Share: