Habari

Vijana wachangamkie fursa za ujasiriamali

15-01-2015

Na Jazaa K. Khamis

Vijana wa jimbo la Magogoni wametakiwa kujikubalisha kufanya kazi za ujasiriamali ili kujiendeleza kimaisha.

Akizungumza na mwandishi wa habari kamanda wa vijana wa jimbo hilo Abass Hassan Juma amesema ni vyema kwa vijana kutotegemea ajira serikalini na badala yake kufanya kazi za ujasiriamali.

Amesema vijana wengi wanajiingiza katika vikundi viovu kutokana na kukosa ajira ya serikali hali inayowapelekea kuendelea kuwepo katika mazingira magumu ya kimaisha.

Kamanda huyo ameeleza kuwa kumekuwepo vikundi mbalimbali vya ushirika vimefanikiwa kutokana na mwamko mkubwa wa wananchi, lakini bado vijana hawako tayari kuelekeza nguvu zao.

Aidha amewataka viongozi kuhakikisha wanashirikiana na wananchi wao katika kuendeleza maendeleo ya majimbo yao na taifa kwa jumla.

Share: