Habari

VP1+VP2 =Nani Mkweli Kuhusu Mswada wa Katiba Mpya?

Maalim Seif Shariff Hamad, VP1, katika serikali ya SMZ (SMZ-GNU) anadai kuwa marekebisho yaliyofanywa na Bunge la Jamhuri ya Muungano, Dodoma yahakuzingatia ‘matakwa/maslahi ya Zanzibar’.

Kwa lugha nyepesi kabisa na ya mkato, Zanzibari haikushirikishwa au kilichotoka Zanzibar kifanyike ndani ya marekebisho hayo, hayakuzingatiwa ipasavyo (incorporated).

Ameyesame haya kila kona ya TZ, kuanzia Kibanda Maiti hadi mitaani anapopata nafasi ya kusema hivyo.

Upande wa pili wa story hii, Balozi Seif Ali iddi, VP2, katika serikali ya SMZ (SMZ-GNU) anasema kuwa alichokiwasilisha yeye Bungeni ni kile walichokifanya kwa pamoja – Waziri wa Sheria wa Zanzibar, Abubakar Khamis Bakari (CUF) na Mwanasheria Mkuu [AG] wa Serikali ya SMZ, Othman Massoud (huyu ni ex-officio).

Balozi wetu, VP2 – naye ameyasema haya kila kona ya TZ anapopata nafasi kusema hivyo. Juzi alikuwa na ziara Pemba (kitosoni kwa CUF!) na aliyasema haya kw aushahidi na kwa kinywa kipana, bila woga, bila kuetetereka.

Sasa, sisi wana-mzalendo — kidogo wengi wenu mmepata madarasa ya hali ya juu sana: tujiulize, tumuamini NANI kati ya hawa wawili (wote ni makamo wa Marais wa SMZ, VP1 na VP2), tabaan Maalim Seif naye alikuwmeo katika vikao hivyo vya kiserikali ya SMZ, AG, na waziri wa sheria, bwana Abubakar Khamis Bakari.

Najua pia kama ni kweli yote hayo, basi itakuwa yamepita, na yamepitishwa na cabinet ya Zanzibar, ambayo Maalim seif anaingia/anahudhuria; na mawaziri wake pia kutoka CUF wanaingia. Minutes za vikao hivi, lazima itakuwa zipo, na Katibu Mkuu Kiongozi, Dr.Abdulhamid Yahya Mzee (VP3) ndio kazi yake kuchukua na kuweka kumbukumbu. Jamani huu ndio utaratibu wa uendeshaji wa serikali.

Ukisoma magazeti, haya utayaona, mgongano wa mawazo huu, ufitinishaji huu, na uumizaji huu wa Zanzibari. Mimi naona kuwa kila mchanganganyiko wa mawazo kama huu unavyojitokeza, basi ndio Zanzibar inazidi kuumia na kupotea katika duru ya dunia, na kuipa nguvu Tanganyika kuimaliza Zanzibar ‘for good’.

Mimi hapa kutokana na kauli mbili hizi zenye ‘kurusha roho’, nimechanganyikiwa, na sijui nikamate wapi. Nimeemewa!

‘which is which’??– anayejua atupe elimu zaidi: ukweli ni upi hasa.

Ila mimi bado bado nimeganda kwenye mawazo yangu ya awali niliyokuwa nikiandika kuwa ‘katiba mpya itaimaliza Zanzibar’, then nilisema tokea lini Warioba awe mtu mkweli au kamati kama ile iwe na uadilifu au bunge la Tanzania — tokea lini liifanyie haki Zanzibar.

Nikasema kuwa ‘nini kazi ya wabunge wa Zanzibar kule Bungeni’, nikasema tena kw aspeed ya 100 miles per hour, kuwa tamaa ya mwisho ni BLW kutuamulia hatma yetu. Siku zile mliniona ‘chiz’/crazy: sasa ukwlei huo hapo, mnapewa uwongo, unakuwa ukweli, na ubabaishaji mwingi.

Nilisema tokea lini Tanzania ikafanya jambo la kitaifa likawa na ukwlei na mashiko kamili — nilitoa mifano mingi.Ipi success story ya national program ya TZ iliyofanikiwa – zote ni utapeli tapeli tu, ujanja ujanja tu, na ubabe ubabe tu. Mwisho wa yote haya; ama litatumika jeshi au polisi na watu watapoteza maisha.

Nani mkweli, nani muongo – basi tufahamishwe, na ikiwezekana mmoja wpao aondoke madarakani (resign) ikithibiti kuwa amelidanganya taifa (zanzibar/perjury). sawa sawa; sawa sawa??

Somehow, nina-taasaf kwa kusema kuwa somehow — abubakar khamis bakari ametupiga bao katika mchakato huu wa katiba, sio mtu wazi.

Share: