Habari

Walioshambulia kwa ngumi, kukaba koo wapanda mahakamani Chakechake

IMEANDIKWA NA MARYAM SALUM, PEMBA

MAHAKAMA ya Wilaya Chake Chake imewapandisha kizimbani watuhumiwa wanne, kwa makosa tofauti ikiwemo la kuumiza mwili na kuharibu mali kijiji cha Vichanje Vitongoji.

Wakisomewa mashitaka yao watuhumiwa hao mbele ya hakimu Ussi Ibrahim, walikana mashitaka hayo na kuiomba mahakama iwapatie dhamana.

‘’Mara baada ya washitakiwa hao kupanda kizimbani wakisubiri taratibu za mahakama, ndipo mwendesha mashitaka Asia Ibrahim, alipodai kua shauri hilo lilipangwa kwa ajili ya kusikilizwa, hivyo naiomba mahakama kupanga tarehe nyengine, kwa vile upande wa mashitaka haukupokea mashahidi’’, alidai.

Hakimu wa mahakama hiyo hakuwa na pingamizi juu ya ombi hilo na kusema kwamba ni vyemba kesi hiyo ikarudi tena Aprili 29 mwaka huu kwa ajili ya kusikilizwa.

Awali kosa la kwanza walilolitenda mtuhumiwa Mafunda Ayoub Hamad miaka 70, akishirikiana na mtuhumiwa mweznake Nassor Abdalla Nassor (Sururu) miaka 50, ambapo bila la halali walimshambulia Abdalla Hamad Bakar kwa kumkaba shingo na kumuangusha chini na kumsababishia maumivu.

Kufanya hivyo ni kosa kisheria kinyume na kifungu cha 230 cha sheria namba 6 ya mwaka 2018 sheria ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Kosa la pili wote kwa pamoja siku hiyo hiyo saa 1:35 asubuhi ambao ni mtuhumiwa Nassor Abdalla Nassor, Samoto Tomas Samoto miaka 44, Ali samoto Tomas miaka 37 na Mafunda Ayoub Hmamd , bila ya halali na kwa pamoja walimshambulia Adam Mohamed Haji kwa kumkaba shingo, kumpiga ngumi na mateke mwilini mwake na kumwangusha, jambo ambalo ni kosa, kinyume na kifungu cha 230 cha sheria ya adhabu, sheria nambar 6 ya mwaka 2018.

Aidha Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa, kosa la tatu kwa watuhumiwa hao, ni kuharibu mali ya Abdalla Hamad Bakar, kwa makusudi waliharibu kwa kuving’oa vikuta vinne vyenye thamani ya shilingi 240,000 kwa makisio.

Kosa la nne kwa washitakiwa hao, ilidaiwa kuwa waliharibu mali kwa makusudi waliharibu kwa kuvikata viatu vya ndara pamoja na kuvunja kioo cha simu aina ya sumsung, vitu vyote hivyo vikiwa na thamani ya shilingi 320,000 kwa makisio mali ya Adam Mohammed Haji.

Kufanya hivyo ni kosa kinyume na kifungu cha 326 (1) cha sheria ya adhabu nambari 6 ya mwaka 2018, sheria ya Zanzibar.

Hakimu wa Mahakama hiyo Ussi Ibrahimu, aliahirisha kesi hiyo hadi April 29, mwaka huu na kuendelea na shitaka lao.

MWISHO.

Share: