Habari

WANANCHI SHEHIA YA MPAPA UNGUJA WATOA YAMAYONI

Imeandikwa na Salmin Juma , Zanzibar
salminjsalmin@gmail.com
0772997018

Wananchi wa shehia ya Mpapa wilaya ya kati unguja wamekishauri chama cha waandishi wa habari wanawake TAMWA – Zanzibar kufanya kila liwezekanalo ili kuendeleza mradi wa kukuza uwajibikaji Zanzibar (Promoting Accountability of Zanzibar) wakidai kuwa umekuja kuwazindua katika kupigania haki zao za msingi.

Walisema, wameanza kusikia kuwa mradi huo unaelekea ukingoni, hivyo wamewaomba TAMWA na washiriki wenzao kuhakikisha mradi unaendelea au unarejea tena kwani hatua kubwa za kimaendeleo wamesifikiwa kupitia mradio huo.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi aliyefika kijijini kwao Mpapa kujionea hali halisi za wananchi katika harakati za kujiletea maendeleo, mwananchi Ali Talib Suleiman alisema, kuingia kwa mradi wa kukuza uwajibikaji shehiani mwao kumesaidia kukubwa wananchi kujitambua hasa katika kupigia mbio mamb yao.

“mwanzo hali ilikua mbaya, hatukuweza kuzungumza, nakisia mradio huu umefanikiwa kwa 60% kutuzindua alau kuweza kusema mambo yetu tunayo yataka” alisema Suleiman.

Akigusia jambo kubwa walilo shikamana wananchi kulitafutia ufumbuzi alisema ni suala la maji, ambayo kwa sasa ijapokua hayapatikani kiukamilifu lakini wamelifikisha suala hilo katika mamlaka husika hasa katika afisi za halmashauri ya wilaya ya kati na wanaamini inawezekana shida hiyo ikawaondokea.

Halima Idrisa Kassim alisema, mradi umewasaidia sana kuwaamsha kujua haki zao na wameshaanza kufikisha vilio vyao katika mamlaka ingawa shida nyengine hazijaanza kutatuliwa lakini hali tofauti na ilivyokua awali.

Kwa upande wake sheha wa shehia ya Mpapa Khalid Yahya Ramadhan alisema, tangia kuwepo mradi wa PAZA shehiani mwake kiwango cha wananchi kuripoti changamoto kimeongozeka.

“karibu kila siku , watu wanakuja afisini kwangu, wanakuja kuulizia mambo mbalimbali nami nayapeleka mamlaka husika na mengine yameshaanza kufanyiwa kazi, kama vile mradio wa hospitali, kwa nguvu zao wananchi walijitolea kujenga na sasa kituo kimefunguliwa alau kwa mapokezi ya humuda ya kwanza, ila bado ni changamoto katika hili tunahitaji juhudi Zaidi kumalizia kituo hiki na matibabu kikamilifu yaendeshwe” alisema Sheha huyo.

Sambamba na hayo aliongeza kuwa, TAMWA na WAHAMAZA wawafikirie kuhusu mradi huo ukiendelea, wananchi watazidi kuchangamka.

Afisa wa maji kutoka halmashauri ya wilaya ya kati Eng Ali Abdu Ali alisema, kumekua na ongezeko la upokeaji wa malalamiko ya wananchi ikiwamo wanaotaka ufafanuzi wa jambo au huduma, hivyo kasi hiyo imepelekea hata watendaji wa serikali kuamka na kuzidisha bidii katika kazi maana hali ni tofauti na zamani.

Alisema, malalamiko wanayoyapokea ni mengi na serikali kupitia mamlaka ya maji inajukumu la kuhakikisha wananchi wake wote wanapata huduma za maji popote walipo na imejipanga kwa hilo, hivyo kwa maeneo ambayo bado hayajafikwa na huduma wawe wastahamilivu juhudi zinafanywa ili kuwafikishia.

Mradi wa kukuza uwajibikaji Zanzibar (Promotingi Accountability of Zanzibar) unatekelezwa na chama cha waandishi wa habari wanawake Tanzania TAMWA – Zanzibar, Jumuiya ya waandishi wa habari za Maendeleo Zanzibar- WAHAMAZA na NGENARECO kwa upande wa Pemba.

Mradi upo katika wilaya sita za Unguja na Pemba, lengo ni kuwaamsha wananchi kuzungumzia haki zao kama vile ukosefu wa huma ya maji, huduma za afya, barabara na nyenginezo, pamoja na kuwafanya watendaji serikalini n ahata taasisi zisizo za kiserikali kuwajibika ipasavyo katika majukumu yao . Mradi wa ulianza Novemba 2017 na unatarajiwa kumalizika Febuari 2019

PembaToday

Share: