Habari

Wananchi waitwa maonesho ya chakula Pemba, Dk Shein mgeni rasmi

October 9, 2018

Imeandikwa na Amina Mmanga, Pemba

KAIMU Waziri wa Kilimo, Maliasili, Uvuvi na Mifugo, Haji Omari Kheri, amewataka wananchi kisiwani Pemba kujitokeza kwa wingi katika maazimisho ya maonesho ya siku ya chakula duniani, yatakayo fanyika Oktoba 11 hadi 18, mwaka huu katika eneo la Shamba la Ufugaji Chamanangwe Wilaya ya Wete Pemba.

Akizungumza na waandishi wa habari katika eneo la maonesho hayo, aliwataka wananchi kutumia fursa hiyo kwa lengo la kuonesha mazao yao pamoja na kupata elimu ya kutumia kilimo na ufuguji bora ili kuweza kujipatia chakula chenye tija .

Alisema lengo hasa la kuazishwa kwa maonesho hayo ni kuwaelimisha wananchi wa Zanzibar hususan Kisiwani Pemba waweze kulima, kufuga, na kupanda kisasa kwa lengo la kuhakikisaha, wanapata chakula chenye tija ili kuondoa tatizo la njaa duniani.

Aidha Kaimu waziri huyo, alisema kuwa kupitia kauli mbiyu ya Kilimo mwaka huu “ni juhudi zetu ndio ndio hatma zetu na dunia bila ya njaa inawezekana ifikapo mwaka 2030” hivyo Serikali imejipanga katika kuweka mikakati itakayo muezesha mkulima na mfugaji kufikia malengo yao .

Alisema kuwa maazimisho hayo yalioshirikisha tasisis zote za kilimo, mali asili, uvuvi na mifufugo ambazo zilikuwa na azma ya kuwafundisha wakulima pamoja na kuwa na uwelewa na utaalamu wa kuendeleza mifugo na kilimo kwa utaalamu zaidi.

Aidha alisema kupitia kwa maonesho hayo wakulima na wajasiri amali watapata fursa ya kuonesha pamoja na kupata soko la kuuza bidha zao katika kipinndi chote.

Akijibu masuali alio ulizwana baadhi ya waaandishi wa habari, Kaimu waziri huyo, alisema serikali imejipanga katika kuweka miundombinu bora na kuhakikisha kauli mbiyu hiyo inafikia lengo lake.

Alifafanua kuwa, serikali imeanzisha mpango madhubuti katika kuelimisha wakulima na wafugaji na katika kufikia hilo, serikali imejipanga kununua matrekta 100 ambayo kwa sasa ina jumla ya matrekta 20 ambayo imenunua na12 ni ya msaada.

Alisema licha yakuweazisha kwa mipango hiyo lakini Serikali imeingia mkataba na Wakorea wa kupata bilioni 100 kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji maji kwa lengo la kumuendeleza mkulima.

“Juhudi kadhaa serikali imekuwa ikizichukua kuhakikisha mkulima wa Zanzibar anazalisha chukula kwa wingi na kuona hakuna hata dalilia ya njaa hapa nchini,”alieleza.

Haya ni maonesha ya kwanza ya chakula kuwahi kufanyika kisiwani Pemba, ambapo manonesha kama hayo yatafanyika yena mwakani katika eneo hilo la Chamanangwe.

Katika ufunguzi wa maonesho hayo ya siku saba mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi dk Ali Mohamed Shein.

PembaToday

Share: