Habari

WANANCHI WAZINDUKA, TAMWA NA WAHAMAZA WANAHUSIKA

WANANCHI WAZINDUKA, TAMWA NA WAHAMAZA WANAHUSIKA
Imeandikwa na Salmin Juma , Zanzibar
salminjsalmin@gmail.com
0772997018

Wananchi kutoka maeneo mbalimbali Kisiwani Unguja wameamua kupaza sauti zao katika changamoto tofauti zinayowakabili kwa lengo la kuishi katika Maisha ya amani na utulivu.

Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi kwa Nyati tofauti wananchi hao walisema, kilicho wafanya kuwa na uthubutu wa kudai haki zao ni mradi wa kukuza uwajibikaji Zanzibar (Promoting Accountability of Zanzibar- PAZA) uliyo wafikia katika maeneo yao.

Mmoja miongoni mwa wananchi hao aliyejitambulisha kwa jina la Fatma Khamis Mussa kutoka shehia ya Mchenza shauri (78) alisema, katika kipindi chote cha nyuma hakuwahi kujua kuandika wala kusoma na hakujaribu kuzungumzia suala hilo lakini tokea kupata elimu katika mradio wa PAZA ameamua kuungana na wenzake kudai haki yao ya elimu na wameshaanza kusoma na kuandika.

“mradi umetusaidia , tulikwenda halmashauri kupeleka kero yetu na wametusikiliza, wakatufungulia darasa la watu wazima na hadi sasa natuweza kuandika na kusoma japo kidogokidogo” alisema mwananchi huyo.

Mwajuma Ali Ussi wa shehia ya Chaani Masingini alifahamisha kuwa, ingawa bado changamoto ya maji haijatatuka vizuri lakini waliamua kupaza sauti na hadi sasa wanaendelea kulilia huduma hiyo katika baadhi ya maeneo irejee vizuri.

Alipoulizwa na mwandishi wa habari hizi juu ya mwamko wa kusemea kero zao wameupata wapi, alikiri kuwa mradi wa PAZA uliwapa nguvu na hamasa zaidi kudai haki zao kwani awali hawakutambua kuwa wanauwezo wa kuziambia mamlaka husika katika yanayowakabili.

Mashamara Chumu Kombo ambae ni afisa elimu wilaya ya kaskazini A alisema, kwa kiwango kikubwa wananchi wa wilaya hiyo wameamka katika elimu.

“wazee wamemka kudai haki ya kusoma pia wanapigia mbio sana watoto wao kuhakikisha wanapata elimu”alisema Afisa huyo.

Alisema, kutokana na mwamko uliyopo wilayani humo anatamani kuona mradi haumaliziki kwani manufaa yake ni makubwa hasa katika sekta ya elimu.

Sheha wa shehia ya Mpapa wilaya ya kati Unguja Khalid Yahya Ramadhani alisema, tokea wnaanchi wapate elimu ya uhamasishwaji wa kupaza sauti zao katika mambo mbalimbali, kiwango cha wananchi kuingia na kutoka kufikisha malalamiko yao kimeongezeka katika afisi yake.

“wananchi sasa wamejitambua, mradi ukimalizika watapata shida, mfano kuhusu maji mara nyingi wananchi wanakuja kutaka kujua tumefikia wapi na hatua zinaendelea kuona jambo hili linatatuka” alisema sheha huyo.

Kwa upande wake Afisa ufatiliaji na tathmini kutoka TAMWA nd: Muhammed Khatib Muhammed alisema, lengo la mradi ni kuhakikisha wananchi wanakuwa na uthubutu wa kuzunguzia changamoto zinazo wakabili kwa lengo la kupatiwa suluhisho ili huduma zilizokatika zirejee kama kawaida.

“pia watendaji katika mamlaka wawajibike ipasavyo kushuhulikia kero za wananchi” alisema Muhammed

Mwandishi wa habari hizi alitembelea katika wilaya zote tatu za unguja ambapo mradi wa PAZA unatekelezwa na kushuhudia wananchi namna walivyo zinduka kuzungumzia kero zao ingawa sio zote zilizotatuka, kama vile huduma ya maji bado haijarejea kikamilifu katika shehia ya chaani masingini, huduma ya afya bado inalalamikiwa katika shehia ya mpapa.

Mradi wa PAZA ulianza Novemba 2017 na unatarajiwa kumalizika Febuari 2019 mradi ambao unatekelezwa katika wilaya tatu za nguja (wilaya ya kaskazini A, wilaya ya kati na wilaya ya kusini ) na Pemba pia upo katika wilaya tatu ( Wilaya ya chakechake, wilaya ya Wete na wilaya na Micheweni)

Mradi unasimamiwa na kutekelezwa na chama cha waandishi wa habari wanawake Tanzaniab-Zanzibar – TAMWA, Jumuiya ya waandishi wa habari za Maendeleo Zanzibar – WAHAMAZA pamoja na NGENARECO kisiwani Pemba.

PembaToday

Share: