Habari

Wapemba Nao Wanahitaji Mitambo ya Redio na TvP.

Wananchi wa Pemba wanajulikana sana kwa Msimamo wao juu ya Maendeleo ya Jamii bila yakusubiri Serikali ya SMZ kuwaletea Maendeleo. Hayo ambayo yameiduwanzisha Pemba na wapemba kuhamia Unyasani na kwengineko kwakujitafutia maisha bora. Wao ni watu wakujituma na kujisomesha kwa hali na mali wala hawaoni tabu kuhamia na kuinvest ktk nchi za watu na kuneemesha watu wengine.

Kwa wale waliobakia kule (UDONGINI PEMBA), wamekua watu waliokinai Umasikini wao na kuwa waaminifu na waungwana kuliko nduguzao wa kisiwa cha  Unguja. Lakini hii haitoshi kuleta mabadiliko ya maendeleo ya Kijamii na uchumi kwakufunga Mikono nakusubiri kazi za Serikali.

Kama ilivokua umaarufu wao juu ya Msimamo na Uchapaji kazi wa Wananchi  wenye asili ya  Pemba. Nifadhali waendelee kutumia sifa hiyo wakati huu ambao tayari wana nyanzo muhimu sana yakuleta mabadiliko ya kisiwa chao na jamii zao.

Nikisema hivi ninamaana kwamba nimepata  Mashaka sana kuona Wapemba Vijana wanajikusanya Jua Kali Chake Chake nakuuza biashara mbovu kutoka China. Au kuuza Bidhaa hizo kwa hizo wakati kuna biashara nyingi tu zisizo za Vitambaa. Tokea walipopatiwa Umeme wa Cable kutoka Tanga kwa  Msaada wa Norway. Ambao waliipatia Serikali ya Tanganyika/ TANZANIA pesa asilimia 731kr. Ni sawa na $ 122 au Billioni 169 Ts.

Msaada huu ukiangalia Reporti ya NORDICS nikuwawezesha Wazanzibari wa Unguja na Pemba  kufanya biashara na kujinasua kiuchumi. Mfano Ni kuletewa Umeme wa uhakika kwa biashara zao, barabara za kisasa, na Maji safi. hayo maji safi na Barabara za kisasa hazikujengwa na badala yake  Wazanzibari wamewqekewa Ulimi wa Paka.

Lakini Umeme wa Uhakika upo Pemba wala haukatwi katwi kama nduguzao wa Unguja. Hivyo Wanatakiwa wapemba watumie fursa hii nakbuni njia nyengine za Biashara badala yakuuza bishara moja pale Chake Chake.  Hii ni itikadi ya misaada ya Nchi za Ulaya wanaposaidia Miradi ya Kimaendeleo kama hii wanataka waone yale Maendeleo yanatumiwa na Wananchi na wanajivunia matunda hayo.

Leo hii unapotembea Pemba utakuta watu wamejikusanya Vikundi wanapiga Bobo vibarazani. Kama vile hakuna lakubuni. Au nikwasababu Hamuna Elimu ya Redio mukaona Jinsi Nchi za Wenzenu kama vile Indonesia, Malasyia, Philipins na kwqengineko wanachangamkia Biashara?.

Nikisema hivyo nimaana kwamba wananchi wa Kisiwa cha Pemba wanaumeme wa uhakika kuliko Unguja. Lakini Bado wanaendelea kuzembea tija hii ya Umeme kwakuendeleza biashara zao. Dala dala za Pemba zinalazwa saa kumi kwa kisingizio ati hawana ABIRIA. Utakuwaje na Abiria wakati gari umeshailaza?

Maduka ya Pemba hata siku za Ramadhani au Sikukuu yanafungwa saa 11 za jioni kwa kisngizio cha kukaa Mbali au hakuna wateja. Hivo Pemba ina umbali kama wa Mkoa wa Temeke to Kinondoni?

Hii yote inatokana na Ufinyu wa maarifa na Elimu mbali mabli za kimaendeleo ambazo kwa uhakika hupatikana kutokana nakuwa na Activ Mdea Broadcasting. Mfano Tv, Redio na hata vyombo vya Sinema. sinashaka huleta Muamsho katika jamii na watu wakaweza kubuni Njia nyengine zakiuchumi. Haya yote yanakosekana katika Visiwa Vyetu vya Unguja na Pemba na ndio maana maendeleo na Mzunguko wa Biashara unakua mdogo sana.

Wazanzibari lazima tukubali kwambva Dunia inabadilika kwa nguvu, na jamii zinakwenda na wakati tulionao wa Technologia na Inovation ya small bisiness. Tumepatiwa umeme kwanini tusiutumie tukazalisha mali, kwakufungua nyenzo mpya za Biashara kama vile Bad & Breakfast hotel. Mikahawa ya kisasa ambayo tuataweza kuuza hata Chai za aina mbali mbali, Bekari za Mikate na Cakes, Vituo vya Computer ambavyo vitawaconect Vijana wetu Duniani,Mashirika ya kushonea nguo za kike na Kiume. Sehemu zakufanyia Massage au kupiga  Chuku. Vituo vyakusomesha watoto, Amusment ndogo ndogo n.k.

Tutake tusitake Nchi zetu ni Visiwa vilivyozungukwa na Bahari zenye fukwe nzuri. Hivo hatuna njia yakupinga utalii kwani ndio njia moja wapo ambayo itatuletea tija na kupanua utamaduni wetu.Lakini tufanye Utalii ambao utalingana na utamaduni wetu, utampatia Mtu binafsi kipoato na maendeleo. Huna haja yakuuza Mvinyo uliokua una ulevi. Kuna Vinywaji vingi ni Non Alcoholoc.

Serikali kwa maana hiyo inawajibu mkubwa wakueneza habari katika mitaandao juu ya Elimu Bora za utalii wa Bad & Breakfast na Biashara nyengine ndogo ndogo. Tutakapo timiza hayo basi Wananchi wa Kisiwa cha Pemba wanaweza wakapata nguvu Mpya za kuendesha biashara zao hadi usiku wa saa 5. Hasa kwa vile Pemba ni nchi ya amani na utulivu basi itafanikiwa katika Mzunguko wa Biashara.

Utalii wa Bad & Breakfast ni utalii wa mtu binafsi ambao Mmiliki atakua ni Mzanzibari Mwenyewe. Utalii huu ndio utalinda zaidi Culture yetu, Dini yetu na kuitangaza Recipies zetu za Vyakula.

Kwanini Serikali ijenge Mtambo wa Redio Fumba na iache hata kufanya matengenezo ule Mtambo wa redio wa Machomane?

Share: