Habari

Wasia wa Ndugu zetu wa (Uamsho) waloko Ndani .

mselem

Mwana Familia

Kawaida kila week hupewa siku moja ya kuweza kuonana na mdogo wetu ambae yuko ndani kwa tuhuma za Kesi ya Ugaidi ( Uamsho) mara nyingi tukionana nae ilikua tunaweza kupata muda angalau wa takika 20 kuweza kuzungumza na wana familia hata kama mbele yetu husimamiwa na Askari wa magereza lakini tunazungumza sana yale mambo yanayo husiana na yeye hali yake na kumuliza hali za wenzake walomo ndani.

Lakini hali ya jana ilitushangaza sana visitors kutokana na ulinzi mkali ulio kuwepo na hawakutaka kuturuhusu sote wana familia kwenda waliruhusu mtu moja tu kwenda na wengine bakie , mimi nilipata bahati hio kwa vile ni kaka mshukiwa na nilingia na kwenda kumuona na kwa bahati yule askari wa Magereza alie tusimamia anafahamiana na mdogo wangu na akamuomba atupe faraha kidogo kuna mambo ya kifamilia tunataka kuzungumza muhimu.

Alikubali na akaondoka kidogo , kikubwa alichonambia nikusema hali ikoje huko uraiani? sisi humu ndani tuna matumaini makubwa Ishallah kwa Uwezo wa M/mungu tukatako na mambo yakabadilika lakini uhakika nikua hali sio mzuru humu na wengi wetu ni wagonjwa na kama unavyo jua kifungo ni gereza na huna uhuru wala husaminiki na hasa gereza zetu hizi za kiafrica na kosa tulilofungiwa ni chuki tu zakisiasa, lakini sisi tunamtegemea Allah zaidi na nyiyi huko nje musitusaliti .

Mimi nikamuliza kusaliti vipi akasema kuipigia kura ccm nisawa na kutusaliti na sisi humu tulimo, Na yoyote atakaye fanya hivyo basi sisi Tumeshamshtaki Allah na tunaomba madua makubwa makubwa yakuweza kumshtakia Allah na zulma zote tunazo fanyia kwahio ikiwa mtu yoyote atatusaliti kwa njia hii au nyingine basi na yeye kashiriki kutukandamiza na atakua hanatafauti yoyote miongoni mwahao waliokua wameasha haki na kuingia katika batli.

Akamalizia kusema tunawaombea uchaguzi mwema huko nje na Ishallah M/mungu atapitisha rehma zake na sisi tutatoka kwa rehma ya Allah.

Terrorism suspects (1)

Familia

Share: