Habari

WASOMI ZANZIBAR WAMGOMEA DOKTA SHEIN

5bf0Ali-Mohamed-Shein

Katika kile kinachoaminika kuwa ni muendelezo wa Wazanzibari kudai haki yao ya msingi ya tarehe 25 October kwa njia za amani wasomi wa vyuo vikuu nao wameungana na Wananchi wa Zanzibar katika kushinikiza kupatikana kwa haki yao iliyoporwa Oktoba 25, 2015 kwa kuigomea serikali ya Dr Shein ambayo imepatikana baada ya kufutwa kwa matokeo ya Uchaguzi na kuitishwa kwa Uchaguzi ulioitwa wa marudio uliofanyika Machi 20, 2016.

Tangu kumalizika kwa Uchaguzi huo ambao ulimpa Dokta Shein asilimia 91% na baadae kuunda Serikali, kumekuwepo na migomo iliyohamasishwa na Chama Cha Wananchi CUF kuisusia Serikali ili kushinikiza kutangazwa kwa matokeo ya tarehe 25 Oktoba ambayo yalimpa Ushindi Mgombea wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad kumzidi mpinzani wake kwa idadi ya kura 25,831 sawa na asilimia 53.40% dhidi ya asilimia 46.00% aalizoambulia Dokta Shein.

Katika hali ambayo inaonekana kufanana na matukio ya kuigomea serikali iliyowekwa kimabavu na kwa kuumia nguvu za dola, Timu ya mpira ya Chuo Cha Kumbumbu ya Al-Sumeit wameamua kugomea kuhudhuria mechi ya ufunguzi ya mashindano ya shirikisho la Wanafunzi wa Elimu ya Juu Zanzibar (ZAHLIFE) ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Dr. Shein. Wanafunzi hao wamedai kuwa hawawezi kuhudhuria katika mechi ya ufunguzi ambayo mgeni rasmi Dokta Shein ndiye mlalamikiwaji mkuu aliyewekwa madarakani kwa kutumia nguvu za kijeshi na Tume ya Uchguzi ya Zanzbar.

zahalife

Pia wanafunzi hao walisema hata Mwenyekiti wa ZAHLIFE ambae ni rais wa Serikali ya Wanafunzi ya Chuo Kikuu cha Zanzibar (SUZA) ameshika madaraka ya serikali hiyo kwa njia zisizoendana na taratibu na kanuni baada ya kulazimisha kubakia madarakani hata baada ya kushindwa kwa njia ya kura.

Pamoja na kuwa timu hiyo iliweka msimamo wa kutohudhuria katika ufunguzi huo timu hiyo ilihudhuria baada ya nguvu na vitisho vikubwa vilivyofanywa na viongozi wa CCM. Hata hivyo wanafunzi hao walisema kuwa haikuwa sahihi kwao kuhudhuria mechi hiyo bali walilazimika kutokana na vitisho na nguvu baada ya kutishiwa kusimamishwa masomo yao.

Mwandishi wa makala hii amefanya mazungumzo na wanafunzi mbali mbali wa Vyuo Vikuu vya Zanzibar, huku wakidai kuwa kwa muda mrefu chaguzi za serikali za Wanafunzi katika vyuo vyao zinatawaliwa na ukiukwaji wa kanuni huku kukiwa na uingiliwaji mkubwa wa Idara za Usalama, Uongozi w vyuo hivyo pamoja na makada na viongozi wa juu wa CCM.

“Tumeweka msimamo wa kuandaa migomo kama hatua ya kuishinikiza serikali kutenda haki, na sisi kama wasomi tunaapa kulisimamia hili mpaka pale haki itakapopatikana” Alisema Mwanafunzi wa Shahada ya Kwanza ya Ualimu kutoka Chuo Kikuu Cha Taifa Cha Zanzibar (SUZA) kwa masharti ya kutotajwa jina lake.

Nae mwanafunzi mwengine alisema kuwa wanafunzi wa chuo cha SUZA wametendewa udhalimu kama alioutenda Dr. Shein kwa Wazanzibari kwa kuwekewa raisi ambaye hawakumchagua na kumpora ushindi wake waliemchagua na kusema kuwa hawana sababu yoyote ya kusita kuwagomea CCM.

Ikumbukwe kuwa SUZA ni chuo cha mwanzo kukumbwa na jinamizi la Jecha Salim Jecha na kupelekea kuwa katika wakati mgumu baada ya alieshinda kuporwa ushindi wake kwa nguvu za dola huku Idara ya Usalama wa Taifa, Jeshi la Polisi na Viongozi wa juu wa CCM wakionekana kushiriki kikamilifu kuvuruga mchakato wa Uchaguzi kwa kulazimisha kuwa mshindi wa Uchaguzi chuoni hapo atoke katika kambi inayoungwa mkono na CCM.

Katika Chuo Cha Uongozi wa Fedha – Chwaka nako hali si shwari baada ya baadhi ya wanafunzi kugoma kushriki katika chakula cha futari ya pamoja kwa kile walichokiita kujitenga na wanafunzi wanaoaminika kuwa ni watoto wa viongozi na wafuasi wa CCM.

Alipoulizwa mmoja wa wanafunzi hao kwa nini mumeamua kuchukua uamuzi hayo? Alijibu “Hapa ndipo CCM ilipotufikisha na kamwe hatutorudi nyuma mpaka wakubali kutenda haki”.

Wanafunzi hao wameendelea kusisitiza msimamo kwa kusema kuwa kwa sasa kitakachoendelea ni mwendo wa mgomo tu popote walipo iwe shule, chuoni, mskitini au majumbani.

CHANZO NA MWANAFUNZI WA CHUO KIKUU SUZA

Share: