AudioHabariHabari-Picha

Watu wanaojuilikana kuwa ni vikosi vya SMZ na wafuasi wa CCM wafanya jinai Tumbatu

VIKOSI VYA HAJI OMARI KHERI VYAONYESHA UBABE NYUMBANI KWAO TUMBATU.

WAFUASI WA CUF WACHOMEWA NYUMBA ZAO NA KUHARIBIWA MALI ZAO TUMBATU MKOA WA KASKAZINI UNGUJA.

Watu wanaojuilikana kuwa ni vikosi vya Serikali ya Zanzibar na wafuasi wa CCM ingawa hujifunika nyuso zao usiku wa Jana walivamia kisiwa cha Tumbatu Zanzibar na kuchoma moto nyumba nyingi na kuharibu mali za watu wanaotambulika kuwa ni wafuasi wa Chama cha CUF. Hivi tukiripoti habari hii familia nyingi za wananchi wa kisiwa hicho hawana sehemu za kukaa na wengi wanahifadhiwa na jamaa zao.

Usiku huohuo wa Jana nyumba pia nyingi zilitiwa alama ya “X” huku mazombi hao wakisikika kuwa watarudi tena kuzichoma nyumba hizo pia.

Haya yanafanyika huku polisi Zanzibar ikionekana kutochukuwa hatua zozote mwafaka kuzuwia vitendo hivi vya unyanyasaji dhidi ya raia wenye kuunga mkono chama cha upinzani.

Leo, Jumamosi tarehe 02/04/2016, Timu ya waandishi wa Habari na wasaidizi wa Sheria walifanya ziara ya kutembelea na kukagua maeneo mbalimbali ya kisiwa cha Tumbatu yaliyovamiwa na kuhujumiwa na Makundi ya watu wanaoendesha uharamia katika maeneo mbalimbali ya Zanzibar.

Katika ziara hiyo, Timu hiyo ilioneshwa maeneo yaliyovunjwa na kutiwa moto na kuteketea kabisa, maeneo yaliyovunjwa na kuibiwa mali zikiwemo fedha taslim na madini ya aina tafauti ikiwemo dhahabu na fedha.

Kwa mujibu wa waathirika wa hujuma hizo, mipango hiyo hupangwa na kutekelezwa kwa kuweka alama maalum ‘x’ katika majumba ya wafuasi wa CUF na kisha kutumiwa baadhi ya viongozi na wanasiasa wa eneo hill la Tumbatu ili kuchochea na kutekeleza hujuma hizi dhidi ya raia wanyonge.

Huu ni mwendelezo wa unyanyasaji unaondelea Zanzibar unaofanywa na Serikali haramu ya Zanzibar ambayo imepewa baraka zote na DIKTETA JOHN POMBE MAGUFULI mkoloni mpya wa Zanzibar.

Tunafanya utaratibu wa kupiga harambee ya kuwachangia ndugu zetu hawa waliofikwa na maafa haya tujue tutawasaidiaje, tutakujulisheni zaidi.

Kwa wale ambao hawakuwahi kuisikiliza audio ya Mahojiano ya DW na mmoja wa Wahanga anaweza kuisikiliza hapo chini.

Chanzo : Mwandishi Wetu

Tagsslider
Share: