Habari

WAVUVI 54 KUTOKA WILAYA YA MICHEWENI WAKAMATWA

Jana siku ya Jumatano tarehe 18/04/2018 majira ya saa nne asubuhi huko ktk bahari ya Msuka wavuvi 54 wamekamatwa na meli ya kikosi cha wana maji cha Tanzania Bara ambao kiujumla wapo ktk maeneo ya bahari upande wa msuka Pemba

Wavuvi hao ambao walikuwa na chombo chao wakitokea Mombasa Kenya ambako walikuweko huko zaidi ya miezi mitatu kwa ajili ya dago

Wakati wamo safarini karibu na kufikia maeneo ya kwao Msuka Pemba meli hio iliwafuata na kuwapa ishara ya kuwa wasimamishe chombo chao ambapo nahoza wa chombo hicho alijifanya kama hajasikia

Baada ya kuona wanakaidi amri hio walipiga honi na kutoa tangazo kuwaomba wasimamishe chombo chao hicho ambapo hatimae walisimama

Walipofika kwenye chombo waliwauliza masuala mengi ikiwemo kuwauliza wanatokea wapi?,
Jee hati za kusafiria mnazo na mengi mengineo

Baada ya mabizano makubwa kati ya wavuvi na wana maji hao hitimisho ni kuwa wameamua kuwachukua vijana hao kwenye meli yao hio hadi Tanga na kukiacha chombo chao ambacho kilishaanza kukimbiwa na maji kwa maana ya kupwewa

Hivi sasa wakati natuma taarifa hii wavuvi hawa wako bandarini Tanga.

Huu ni uonevu mkubwa usioweza kuvumilka nchi moja lakini raia wake tunanyanyasana kiasi hichi bila ya sababu za msingi

Kiujumla wavuvi wanapotoka hapa Pemba kwenda dago Kenya wote hulazimika kukata hati za dharura za kusafiria na huondoka hapa kihalali kabisa

Baadhi ya vijana hao ambao nimebahatika kupata majina yao kupitia wazee wao hapo kijijini kwao Kichaka Pumu Msuka jimbo la Konde ni hawa wafuatao:-
1.HAMAD SAID NASSOR 35 YRS
2.ALI SALIM NASSOR 25 YRS
3.MOH’D HAMAD MUSSA 24 YRS
4.SAID MAKAME FAKI 21 YRS
5.HAMAD MAKAME FAKI 45 YRS
6.SULEIMAN MBAROUK KHAMIS 22 YRS
7.JUMA KOMBO JUMA 18 YRS
8.SAID FAKI SIMBA 25 YRS

Wavuvi wote hawa ni wakaazi halali wa majimbo ya Konde na Micheweni Pemba ambapo suala hili ni tayari limesharipotiwa kwa waheshimiwa wabunge wa majimbo husika Mhe Khatib Said Haji (OBAMA) Konde na Mhe Haji Khatib Kai kwa ufuatiliaji zaidi ambapo bila kusita wameahidi kulifanyia kazi kwa nguvu zao zote kwani wana uhakika kuwa hao ni wavuvi na wamefuata taratibu zote za kuondoka kwao kimavuvi

Imetolewa na

MKURUGENZI WA HAKI ZA BINADAMU NA SHERIA WILAYA YA MICHEWENI PEMBA.

Mhe.Kombo Mwinyi Shehe.

Share: