Habari

Wawakilishi waishangaa Serikali kutilia nguvu mradi wa camera

Wawakilishi waishangaa Serikali kuelekeza nguvu kwenye mradi wa camera badala ya miradi mengine ya maendeleo.
Wajumbe wa Baraza la wawakilishi wameeleza wasiwasi wao juu ya kutumika vibaya Fedha zilizotengwa kwa ajili ya kuweka camera za CCTV katika baadhi ya naeneo ya Manispaa ya mji wa Zanzibar.

Wakichangia hutuba ya Makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya tawala za mikoa na Idara Maalumu,Wajumbe hao wamesema Fedha hizo zinahitajika kuelekezwa katika shughuli nyengine za maendeleo ikiwemo kuimarisha kwa miradi ya maji safi na salama pamoja na kununulia mashine ya DNA itasadia kuondoa matatizo yanayowakabili wananchi.

Wamesema kwa sasa kuna mambo muhimu katika jamii yanayohitaji kupatiwa ufumbuzi hivyo ni vyema kwa serikali kutekeleza vipaumbele vyake ikwemo kuimarisha mapambano dhidi ya udhalilishaji wa kijinsia na Watoto katika kuhakikisha mashine ya DNA inanunuliwa.

Aidha wametowa wito kwa serikali kuangalia kwa kina masuala ya matumizi bora ya Fedha wakati wa kupanga bajeti za maendeleo ya ili kupunguza malalamiko kwa wananchi.

Jumla ya Fedha Billioni 18 zimekusudiwa kutumika katika mradi wa ufungaji wa Camera za Usalama ambapo kwa sasa mradi huo umeomba kuengezewa Fedha zaidi.

Chanzo: Zanzibar24
……………………………………………………..
Sauti Ya Wazanzibar

Share: