Habari

Wazalishaji wa Majani ya Chai Pemba watoa ya moyoni

November 6, 2018 – by Manager

Imeandikwa na Salmin Juma Salmin, Pemba

email : salminjsalmin@gmail.com

Tel : +255772997018

Serikali na wadau wengine wa maendeleo nchini wametakiwa kuwatazama wajasiriamali kwa jicho la maendeleo ili kufikia malengo waliyoyakusudia.

Hayo yameelezwa na M/kiti wa kikundi cha ushirika cha “Nguvu yetu ni umoja” Maulid Saleh Hamad ambao wanajishuhulisha na uzalishaji wa majani ya Chai kutoka Kiuyu Minungwini mkoa wa kaskazini Pemba.

Machani ya chai aina ya HERBAL TEA yanayozaliwa na kikundi cha NGUVU YETU NI UMOJA WETU cha Kiuyu Pemba
Alisema, ni siku chache tu tangu walipoamua kuanzisha uzalishaji wa majani ya chai na hadi hivi sasa wameshaanza kuona tija yake lakini wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwamo kutoka na ofisi hali ambayo inawarudisha nyuma katika harakati zao hizo.

“ingawa tunafanya kazi lakini tunakabiliwa na changamoto nyingi, mfano hatuna ofisi rasmi, tunahitaji mashine za kisasa za kutengenezea majani ya chai na hata pesa za kuendeshea shuhuli zetu ni kikwazo” alisema Mwenyekiti huyo.

Mwenyekiti wa kikundi cha ushirika cha “Nguvu yetu ni umoja” Maulid Saleh Hamad akiwa amepakata chupa za majani ya chai huku akimsikiliza mwandishi wa habari aliyekuwa akimuuliza suala wakati huo.
Wakizungumzia jinsi walivyo kuwa kiuchumia kutokana na harakati zao hizo M/kiti wa kikundi hicho aalisema, hivi sasa anajimudu na maisha yake tofauti na hali ilivyokuwa awali.

“mwanamke namudu mahitaji yangu ya nyumbani, nimeshanunua kiwanja kupitia kazi hizi na kwa pesa ndogondogo huwa ninazo nashukuru hadi sasa” alisema

Mshika fedha wa kikundi hicho Chumu Hamad Khatib akionyesha bishaa yao ya majani ya chai wanayoyazalisha
Kwa uapande wake Mshika fedha wa kikundi hicho aliyejitambulisha kwa jina la Chumu Hamad Khatib alisema, anafaidika sana na shuhuli hizo ikiwamo kusomesha wanawe na mambo mengineyo.

“ sina mume, najishuhulikia mwenyewe, nashukuru wanangu nawasomesha kupitia pirika hizi hizi” alifahamisha

Chama cha waandishi wa habari wanawake Tanzania TAMWA ambao ndio wanaowashuhulikia akina mama hao kimesema kupitia mratibu wake Asha Mussa Omar wamekua wadau wakubwa wa kuwashika mkono wanawake kwakua muda mrefu walionekana wapo nyuma.

Alisema “ tumeona ni jambo jema kuinua hali za akina mama kwani kumuwezesha mwanamke mmoja ni sawa na kuiwezesha jamii nzima, hivyo atakachokipata kitasaidia sana jamii” alisema Asha.

Pamoja na hayo alisema, katika kuwakuza wajasiriamali TAMWA wametengeneza kamati za biashara na jukumu lake ni kutafuta masoko sehemu mbalimbali ikiwamo katika hoteli kubwa za kitalii pamoja na kuweka masoko ya wazi kwa lengo kuzidi kuzitangaza bishaa hizo.

Akizungumza changamoto zinazowakabili wajasiriamali hao alisema, wanazifahamu na siku zote wamo katika mchakato wa kuzitafutia ufumbuzi wakishikiana na wadau wengine ili lengo la kila mjasiriali lifikiwe.

MWISHO

PembaToday

Share: